Mimba

Hongera, baada ya kuona dalili za mimba sasa unaingia mlongo wa kwanza wa ujauzito. Mlongo wa kwanza wa ujauzito ni miezi mitatu ya mwanzo tangu ushike mimba, pia inajulikana kama wiki ya 1 kuendelea mpaka wiki 12. Wakati wa kipindi hichi mwili wako unaanza mabadiliko mbalimbali, kati ya dalili halisi za mimba ni pamoja na kujisikia kutapika, uchovu wa ajabu, kuumwa kwa mgongo, kubadilika kwa tabia ghafla na stress. Hizi zote ni kawaida kwa mama mjamzito wakati wa wiki ya 1 hadi 12 ya mimba. Kwa bahati nzuri, nyingi ya dalili hizi huwa zinapotea unapoingia kwenye mlongo wa pili wa ujauzito. Unashauliwa kuacha kuvuta sigara na kunywa pombe wakati ukiwa mjamzito, kwani tabia hizi zinaweza mduru mtoto akiwa tumboni.

Wanawake wengi huenda kuona waganga wao (doctors) kipindi hiki cha mlongo wa kwanza mara nyingi wiki ya 8 hadi 10, hii ni vizuri kwani ndio wakati wa muhimu sana kwa mtoto kukuzwa vizuri tumboni. Mganga wako atakuelewesha na kuchukua vipimo vinavyotakiwa kuhakikisha kama kweli una mimba. Wanawake wengi wanaweza pia kusikia mapigo ya moyo ya mtoto akiwa karibu wiki 12 tumboni, ingawa inaweza chukua muda zaidi kwa wanawake wengine.

Wiki ya 1 na 2

Wiki hii ni mara ya mwisho kuona siku zako kabla hujagundua kwamba una mimba. Furahia! sawa, labda hautafurahia kutegemea na matakwa yako. Basi, hiki ni kipindi cha kuaga yale maumivu ya siku (period pains) mpaka utakapojifungua. Kwa wiki hizi mbili za mwanzo mimba bado hata haijashika kwanza. Wakati mganga wako anapohesabu siku yako ya kujifungua huwa anahesabu wiki 40 kuanzia siku yako ya kwanza ya kuona mwezi(period) kabla tuu ya kushika na mimba. Na sio kuanzia siku mimba iliposhika (mara nyingi ni siku ya 14 baada ya kuona mwezi).

Kipindi hiki yai linajiandaa kushuka ili kukutana na mbegu za kiume kutunga ujauzito. Kama unapanga kupata ujauzito, sasa ni wakati muafaka wa kuacha sigara na pombe, pia unaweza anza kunywa vidonge vya vitamin na folic acid, ambavyo husaidia mtoto asipate magonjwa ya ubongo akiwa tumboni.



Wiki ya 3 na 4

Kipindi hichi mwili unatoa hormone zinazoitwa estrogen na progesterone kwa kuuandaa mwili kwa ajili ya siku(period), wakati ovaries zinaporuhusu yai kutoka. Kama ni bahati yako, yai hili ndilo litatunga ujauzito na kusafilishwa kwenda kwenye falopian tube mpaka kwenye uterus na hapo litakaa kwa wiki 40 likitunga mtoto.

Mwili wako

Hongera, inawezekana bado hujui lakini una mimba. Ingawa hauhisi chochote bado mwili wako tayari unafanya kazi kwa kasi kujiandaa kwa ajili ya miezi tisa ijayo.

Nini Kinafanyika ndani ya kizazi(Uterus)

Kizazi kawaida kina uzito wa 60g na 7.5cm kwa urefu, Lakini pindi tuu uzazi unapotunga kinaongezeka kwa ajili ya uongezefu wa hormone inayoitwa oestrogen ambayo inatolewa na placenta. Hormone hii ni muhimu kwani ndio inayo saidia kutengenezwa na kukuza kwa mtoto tumboni, viungo kama mapafu, maini, kidney n.k havitakomaa pasipo hii hormone. Uzazi unanenepa na kusababisha layer kubwa ya majimaji ambayo ndipo mtoto atakapoishi na kukua kwa kipindi chote cha ujauzito. kipindi hichohicho muscle fibers zinajijenga kujiandaa kuzaliwa kwa mtoto.


Nini kinafanyika kwenye shingo ya uzazi (Cervix)

Shingo inaongezeka kidogo kwa upana, inarainika na rangi yake kuwa nyeusi zaidi kuliko kawaida sababu ya kuongezeka kwa uwingi wa mishipa ya damu kwenye eneo hilo. Glands kwenye cervix inajenga ute mzito (Mucus plug) kugundisha shingo ya kizazi ili kisipatwe na maradhi kumkinga mtoto akiwa tumboni.

Kwa kipidi hichi chote hautoona hedhi mpaka ujifungue.