Wednesday 24 October 2012

Mimba wiki ya 7 na 8

Mtoto

Mtoto tumboni anaendelea kukua  na ni mara 10000 kwa ukubwa kuliko alivyokuwa kipindi mimba inatunga. Kiasi kikubwa cha ukuaji ni ujengaji wa kichwa cha mtoto kwani sasa celli mpya za ubongo zinatengenezwa. mdomo na ulimi vinatengenezwa pamoja na miguu na mikono na maini yanajiandaa kufanya kazi yake pia.

Mwili wako

Unapofikia hapa kifua kinakuwa kimeshaongezeka kwa ukubwa, hormones zimeongezeka ka kasi kali na utakuwa umeshaongezeka kwa unene pia.
Chakula bado utakiona kibaya na hata unaweza tapika ukisikia Harufu ya chakula. Jaribu kula chakula ambacho hakikuchefui kwa kipindi hiki.
Pia utatumia muda wako mwingi chooni siku hizi, Hormone inayoitwa hCG inaongeza upitishaji wa damu maeneo ya pelvis (kwa wale wanaopenda fanya mapenzi, huu ndo wakati muafaka) na hii husababisha kutaka kwenda choo ndogo mara kwa mara. Bado unahitaji kunywa maji/juice nyingi sana kwani wote wawili mnahitaji kimiminika mwilini.  Watu wengi huwa wanajisikia vibaya kwa sababu ya kuishiwa na damu ama maji mwilini, hii hali inasabisha wajisikie kuzimia na kuanguka. Pia sijui kama ni kweli, eti wanasema kama unaumwa sana kipindi cha mlongo wa kwanza basi mtoto ni wa kike, hii inatokana na hormone za kike za mama pamoja na za mtoto wa kike tumboni zinakuwa nyingi zaidi kuliko kama ungekuwa na mtoto wa kiume, kwani mtoto wa kiume hatoi hormone hizo kwa wingi.
Uchovu ni kitu kingine cha kuwa makini nacho, kula chakula kidogokidogo mara kwa mara inasaidia kukupatia nguvu mwilini. 

Pia unaweza kuwa na mate mengi mdomoni, hii ni kwa mlongo wa kwanza tuu lakini ni ya kupita tuu, jaribu kula chewing gum zisizo na sukari zinaweza saidia.

Kiungulia ni tatizo jingine unaloweza kupata kipindi hiki, jaribu kutokula chakula chenye spicy nyingi kama pilipili, chakula cha fat nyingi, chakula cha cafeine kama kahawa. Pia, jaribu kutokumywa maji kabla/mara tuu ya kula chakula kwani mchanganyiko wa maji na chakula tumboni unasababisha kiungulia.

Ukosaji wa choo ni tatizo jingine kipindi hiki, mimba inasababisha mishipa kwanye sehemu ya choo kikubwa i-relax na kuruhusu kinyesi kibaki tumboni kwa mda mrefu, hivyo hujikusanya kwa wingi na siku utakapopata choo kinakuwa ni kigumu sana.maziwa mgando na papai lililoiva sana vinaweza saidia.


No comments:

Post a Comment