Sunday 9 November 2014

FUNGUS WAKATI WA MIMBA (Thrush)



Ni kawaida kabisa kutokwa na majimaji mazito (vaginal discharge) ukeni wakati ukiwa na ujazito.  Usiwe na wasiwasi kama majimaji haya ni myepesi na yana muonekano wa rangi ya maziwa.

Dalili za kuwa na fungus ukeni:

·         Majimaji yakiwa mazito, myeupe na rangi ya maziwa, na yanayoonekana kama cottage cheese, ama maziwa ya mgando, ama yaliyoharibika.
·         Kama unawashwa, na kusikia kuvimba kama vile umejikwaruza, na muonekano wa uwekundu sehemu ya ukeni.
·         Inauma wakati wa kujamiiana
·         Unasikia kuchomwachomwa wakati unakojoa

Je nilipataje thrush:

Maambukizi ya ukeni wakati wa mimba ni ya kawaida. Thrush husababishwa na fungus  (yeast) wanaoitwa candida albicans ambao wapo na huishi kwenye miili yetu bila kusababisha tatizo lolote. Wapo pia kwenye mfumo wa chakula na mara nyingi hawana madhara yoyote kwetu na wala hautojua kama wapo.
Huwa wanaleta tatizo pale tuu wakati fungus hawa na vijidudu vingine ndani na nje ya mwili vinapopungua ama kuongezeka kuliko kiasi kinachitakiwa.  Unaweza kupata thrush pale ambapo:
·         Unapokuwa mjamzito mabadiliko ya hormones  kwenye mwili  husababisha mwili uwe na sukari nyingi kuliko kiasi inayoitwa glycogen ambayo husababisha fungus kuzaliana kwa wingi (wanatumia glycogen kama chakula na hivyo kuwapatia nguvu ya kujiongeza idadi).
·         Unapotumia antibiotics, dawa hizi huua vijidudu mwilini ambapo pia huua vijidudu vizuri vinavyopigana na vile vibaya, hivyo basi balance ya vijidudu hivi inakuwa imebadilika na hiyo kusabaisha vile vibaya vizaliane kwa nguvu.
·         Kisukari (Diabetes): kama una ugonjwa wa kisukari ambacho huujakicontrol pia husababisha thrush.
·         Kama immune system yako ni dhoofu. Hii inaweza kutokana na pia na matibabu ya magonjwa kama sarakani (cancer) ama magojwa na HIV.
Ingawa thrush sio magonjwa ya zinaa, yanawezekana kuambukizwa kama partner wako amepata maambukizi haya, hivyo mnashauriwa wote wawili mpate matibabu kwa wakati moja.

Kama unafikiria una thrush, tafadhari mwone daktari.

Daktari atakupatia dawa, ingawa wanashauri kutotumia chochote kipindi cha mlongo wa kwanza wa mimba (miezi 3 ya mwanzo) .
Dawa zingine ni za kuweka ukeni (kidonge), unashauriwa kuweka usiku wakati umelala ili inyonywe vizuri wakati umelala. Thrush ni vigumu kupona upesi hivyo basi ni vyema umalize dozi utakayopewa na daktari.  Tafadhari usichukue dawa za vidonge ambayo utahitaji kumeza, bado haijajulikana kama vina madhara gani kwa mtoto.

Je nifanyeje

·         Wakati unapojiosha ukeni, usitumie sabuni osha na maji masafi (sio ya kisima) ikiwezekana jichemshia maji kidogo tuu(kuua vijidudu) kwa ajili ukeni. Na ikiwezekana jioshe mara moja kwa siku kwani kujisafisha sana ukeni unaondoa wale wadudu wanaohitajika kulinda uke (Good Flora microorganism).
·         Usitumie mafuta yatakayoirritate ngozi kama pedi za kunukia, deodorant za ukeni, na  sabuni zakunukia.
·         Kula maziwa mgando yasiyo na sukari, ama ingiza maziwa ya mgando ukeni.
·         Kama utatumia maziwa mgando, njia rahisi ya kuweka ukeni ni kwa kutumia tampoo, chovya tampoo kwenye maziwa mgando, dumbukiza tampoo ukeni, iache kwa muda wa lisaa limoja, alafu itoe.
·         Kupunguza kueneza thrush, basi jifute toka mbele kwenda nyuma kila baada ya kutumia choo.
·         Vaa chupi za cotton 100%
·         Wakati wa kujamiiana tumia kilainisho(lubricant) kupunguza maumivu kama una thrush.

Je thrush itamfikia mtoto tumboni

Hapana, mtoto amefunikwa na mfuko na hatadhurika.
Hata hivyo ni muhimu kupata matibabu kabla ya kujifungua, kwani mtoto anaweza kuambukizwa wakati akitokea ukeni.
Kama hii ikitokea basi utahitaji matibabu wewe na mtoto, mtoto mara nyingi anakuwa na utando mweupe kwenye ulimi.
Utagundua thrush huja na kuondoka wakati wa mimba, na huchukua mda mrefu kuitibu lakini sio kitu cha kuogopa sana.






3 comments:

  1. Dah! Nashukuru sana mke wangu ana tatizo hili na linaogopesha sana lkn kwa elimu yako nimefarijika. Ubarikiwe sana doctor.

    ReplyDelete
  2. Asanteee docta me hii hali napitia nimepewa dawa lkn hali imerudi vilevile,, nifanyaaje?

    ReplyDelete
  3. Jeee. Haiathiri afya ya mtoyo

    ReplyDelete