Sunday 9 November 2014

FUNGUS WAKATI WA MIMBA (Thrush)



Ni kawaida kabisa kutokwa na majimaji mazito (vaginal discharge) ukeni wakati ukiwa na ujazito.  Usiwe na wasiwasi kama majimaji haya ni myepesi na yana muonekano wa rangi ya maziwa.

Dalili za kuwa na fungus ukeni:

·         Majimaji yakiwa mazito, myeupe na rangi ya maziwa, na yanayoonekana kama cottage cheese, ama maziwa ya mgando, ama yaliyoharibika.
·         Kama unawashwa, na kusikia kuvimba kama vile umejikwaruza, na muonekano wa uwekundu sehemu ya ukeni.
·         Inauma wakati wa kujamiiana
·         Unasikia kuchomwachomwa wakati unakojoa

Je nilipataje thrush:

Maambukizi ya ukeni wakati wa mimba ni ya kawaida. Thrush husababishwa na fungus  (yeast) wanaoitwa candida albicans ambao wapo na huishi kwenye miili yetu bila kusababisha tatizo lolote. Wapo pia kwenye mfumo wa chakula na mara nyingi hawana madhara yoyote kwetu na wala hautojua kama wapo.
Huwa wanaleta tatizo pale tuu wakati fungus hawa na vijidudu vingine ndani na nje ya mwili vinapopungua ama kuongezeka kuliko kiasi kinachitakiwa.  Unaweza kupata thrush pale ambapo:
·         Unapokuwa mjamzito mabadiliko ya hormones  kwenye mwili  husababisha mwili uwe na sukari nyingi kuliko kiasi inayoitwa glycogen ambayo husababisha fungus kuzaliana kwa wingi (wanatumia glycogen kama chakula na hivyo kuwapatia nguvu ya kujiongeza idadi).
·         Unapotumia antibiotics, dawa hizi huua vijidudu mwilini ambapo pia huua vijidudu vizuri vinavyopigana na vile vibaya, hivyo basi balance ya vijidudu hivi inakuwa imebadilika na hiyo kusabaisha vile vibaya vizaliane kwa nguvu.
·         Kisukari (Diabetes): kama una ugonjwa wa kisukari ambacho huujakicontrol pia husababisha thrush.
·         Kama immune system yako ni dhoofu. Hii inaweza kutokana na pia na matibabu ya magonjwa kama sarakani (cancer) ama magojwa na HIV.
Ingawa thrush sio magonjwa ya zinaa, yanawezekana kuambukizwa kama partner wako amepata maambukizi haya, hivyo mnashauriwa wote wawili mpate matibabu kwa wakati moja.

Kama unafikiria una thrush, tafadhari mwone daktari.

Daktari atakupatia dawa, ingawa wanashauri kutotumia chochote kipindi cha mlongo wa kwanza wa mimba (miezi 3 ya mwanzo) .
Dawa zingine ni za kuweka ukeni (kidonge), unashauriwa kuweka usiku wakati umelala ili inyonywe vizuri wakati umelala. Thrush ni vigumu kupona upesi hivyo basi ni vyema umalize dozi utakayopewa na daktari.  Tafadhari usichukue dawa za vidonge ambayo utahitaji kumeza, bado haijajulikana kama vina madhara gani kwa mtoto.

Je nifanyeje

·         Wakati unapojiosha ukeni, usitumie sabuni osha na maji masafi (sio ya kisima) ikiwezekana jichemshia maji kidogo tuu(kuua vijidudu) kwa ajili ukeni. Na ikiwezekana jioshe mara moja kwa siku kwani kujisafisha sana ukeni unaondoa wale wadudu wanaohitajika kulinda uke (Good Flora microorganism).
·         Usitumie mafuta yatakayoirritate ngozi kama pedi za kunukia, deodorant za ukeni, na  sabuni zakunukia.
·         Kula maziwa mgando yasiyo na sukari, ama ingiza maziwa ya mgando ukeni.
·         Kama utatumia maziwa mgando, njia rahisi ya kuweka ukeni ni kwa kutumia tampoo, chovya tampoo kwenye maziwa mgando, dumbukiza tampoo ukeni, iache kwa muda wa lisaa limoja, alafu itoe.
·         Kupunguza kueneza thrush, basi jifute toka mbele kwenda nyuma kila baada ya kutumia choo.
·         Vaa chupi za cotton 100%
·         Wakati wa kujamiiana tumia kilainisho(lubricant) kupunguza maumivu kama una thrush.

Je thrush itamfikia mtoto tumboni

Hapana, mtoto amefunikwa na mfuko na hatadhurika.
Hata hivyo ni muhimu kupata matibabu kabla ya kujifungua, kwani mtoto anaweza kuambukizwa wakati akitokea ukeni.
Kama hii ikitokea basi utahitaji matibabu wewe na mtoto, mtoto mara nyingi anakuwa na utando mweupe kwenye ulimi.
Utagundua thrush huja na kuondoka wakati wa mimba, na huchukua mda mrefu kuitibu lakini sio kitu cha kuogopa sana.






Saturday 8 November 2014

Ugonjwa wa kifafa (seizures) kwa watoto


Kifafa mara nyingi husababishwa na uvujaji wa wave za kama za umeme (electrical discharge) kwenye ubongo ama husababishwa na hali ya kuzimia (baada ya kupunguka kwa msukumo wa damu ubongoni). Dalili (symptoms) zinaweza hutofautiana kulingana na sehemu ipi ya ubongo imehusika, lakini mara nyingi utasikia hali ya mwili kusisimka sio kwa kawaida, misuli kuvutika/kukaza yenyewe, na pia kupoteza fahamu.
Baadhi ya vifafa vingine huwa ni matokeo ya magojwa mengine mwilini, kama upungufu wa sukari kwenye damu, maambukizi, kuuumia kichwa(head injuries), ajari za barabarani au kuoverdose madawa ya kulevya.  Pia kifafa kinaweza sababishwa na uvimbe kwenye ubongo ama tatizo linguine la afya linaloathiri ubongo. Kifafa mara nyingi hutokea zaidi ya mara moja.

Watoto wa chini ya miaka 5 huwa wanapata hali ya kifafa pale joto lao la mwili linapozidi degree 38 (100.4° F (38° C) aina hii ya kifafa inaitwa  Febrile seizure. Hii inaogopesha kama mzazi lakini hii hali ni ya dakika chache tuu, mara chache husababisha matatizo makubwa, especially kama joto hili limesababishwa na maambukizi kama meningitis.

Kwa watoto chini ya miaka 5, kuhold pumzi inaweza sababisha hali ya kifafa (seizure). Kuna watoto wakati wanapokasirika huwa wanashikiria pumzi (hawavuti pumzi kwa sekunde chache) kabla tuu ya kuachia kilio kikubwa, kabla ya kupoteza fahamu kifafa kufuatia. Mara nyingi hali hii huisha yenyewe.

Watoto wa umri zaidi ya miaka 5 wachache huwa na hali hii lakini mara nyingi huwa inaisha baada ya sekunde chache.

Kama mtoto wako ana kifafa ufanyeje
Kama mtoto wako amepatwa na kifafa basi unashauriwa kumlaza chini sehemu ambayo ni salama, wanashauri umlaze upande wake wa kulia. Ondoa kitu chochote cha hatari ambacho kipo karibu, kama vyupa, sindano, mawe n.k. Kama ana cheni shongoni ivue ama kama nguo ipo shingoni ivue pia isimkabe.  Usijaribu kupanua mdomo wa mtoto anapokuwa na kifafa ama kuweka kitu mdomoni kwake, pia usijaribu kuzuia kuweweseka kwake.
Mara tuu kifafa kinapoisha basi mfariji mtoto, ni muhimu kwa watoto kubaki kulala chini mpaka hali hii iishe kabisa nay eye mwenyewe akitaka kuinuka.
Tafadhari mwite daktari pale ambapo kifafa kinaendelea zaidi ya dakika 5, pia kama mtoto ana vitu vifuatavyo:
       . anashindwa kupumua
       .ameumia kichwa
       .ana magonjwa ya moyo
       .hajawahi kupata kifafa zamani
       .kama amekunywa sumu ama ameoverdose dawa.

Baada ya kifafa, mtoto huonekana kuchoka, amechanganyikiwa, na anaweza kulala usingizi mzito sana (postictal period) hauhitaji kumwamsha mtoto as long as anapumua vizuri. Usijaribu kump chakula mpaka mtoto aamke na aonekane kuchangamka.

Baada ya kifafa mtaarifu daktari kuangalia tatizo lililosababisha hiyo hali ni nini.