Tuesday 2 December 2014

Kutapika na Kuharisha kwa watoto

Ni kawaida kwa watoto wachanga na watoto kutapika. Katika kesi nyingi , kutapika hudumu kati ya siku moja mpaka mbili na si ishara ya kitu chochote kikubwa . Kawaida sababu ya kutapika kwa watoto ni gastroenteritis . Haya ni maambukizi ya kolomeo kawaida husababishwa na virusi au bakteria. Na pia husababisha kuhara . Mfumo wa kinga ya mtoto wako kwa kawaida hupigana na maambukizi baada ya siku chache.

Watoto mara nyingi pia hutapika wakati wanapomeza  hewa wakati wa kulishwa . Hata hivyo , kuendelea kutapika wakati mwingine inaweza kuwa ni ishara ya kitu kibaya zaidi , ikiwa ni pamoja maambukizi makali kama vile uti wa mgongo.

Ukurasa huu unaeleza nini cha kufanya kama mtoto wako anaendelea kutapika na iuaelezea baadhi ya sababu ya kawaida ya kutapika kwa watoto wachanga, na watoto kwa ujumla . Kama mtoto wako ana joto la juu , unaweza pia kusoma kuhusu homa kwa watoto

Nini cha kufanya.

Kama mtoto wako anatapika, unapaswa kufuatilia hali kwa uangalifu mkubwa. Amini moyo wako na mpeleke kwa dakitari wako mara moja kama wewe una wasiwasi.

Kama sababu ni tummy bug tuu (kuhara kwa kawaida kwa mtoto ama tummy flu), atakula na kucheza kama kawaida.  Katika kesi hiyo, endelea kumlisha kama kawaida na kumpatia kinywaji (maji, juice n.k) mara kwa mara. Maji humsaidia kutopunguka kwa uwingi wa maji mwilini ambao ni hatari.

Lakini kama haonekani  wa kawaida, - kwa mfano, kama yupo floppy , hasira , kutojibu, au amepoteza hamu ya kula -  inawezekana anaumwa, hivyo unapaswa kuwasiliana na daktari wako mara moja.


Kumpeleka kwa daktari

Unapaswa kuwasiliana na daktari wako kama :

          •Mtoto wako amekuwa akitapika kwa zaidi ya masaa 24
          • Mtoto wako  anatapika  ndani ya masaa nane, au kama unafikiri amepungukiwa na
            maji mwilini.
          • Kama ni floppy, mwnye  hasira, anagoma chakula , au hayupo kwenye hali ya kawaida
,         • Ana maumivu makali tummy
          • Ana maumivu ya kichwa na shingo ngumu.

Ishara ya upungufu wa maji mwilini
Kutapika  kali na kuhara kunaweza kwa urahisi kusababisha upungufu wa maji mwilini , hasa katika
watoto wachanga. Hii ina maana mwili wa mtoto wako hana maji ya kutosha mwilini  au hana chumvi inayohitajika kwa ajili ya mwili kufanya kazi kwa kawaida .

Watoto wenye upungufu wa maji  mara nyingi hujisikia na huonekana kuumwa.

 Ishara ya upungufu wa maji mwilini ni :
• kinywa kikavu
• kilio bila kutoa machozi
• kukojoa kidogo sana au kiasi cha nappies anazokojolea kupunguka.
• Kuongezeka kwa kiu
• Kudhoofika

Ufanyaje

Jambo muhimu zaidi unaweza kufanya kama mtoto wako anatapika ni kuhakikisha anaendelea kunywa maji ya kunywa.
Kama mtoto wako anatapika , endelea kumnyonyesha. Kama wamepungukiwa maji, , atakuwa anahitaji maji ya ziada. Uliza mfamasia wako kama wangeweza kupendekeza kumpatia dawa ya kusaidia kutopunguka kwa maji mwilini.
Dawa hii ni poda maalum unaitengeneza kwa kuweka kwenye maji. Ina sukari na chumvi katika kiasi maalum ya kusaidia kuchukua nafasi ya maji na chumvi kupotea kwa njia ya kutapika na kuhara.
Watoto ambao hutapika wanapaswa kunywa maji haya kidogokidogo hivyo hawatapungukiwa maji
mwilini. .Pia motto anaweza kunywa maji , maji mengi kwenye juice ya kuchanganya na maji , diluted maji ya matunda au maziwa.
Hata hivyo, kama pia wanaharisha, maji ya matunda  ziepukwe. Tena, GP wako au mfamasia anaweza kupendekeza ORS.


Dawa ya kusaidia wakati wa kuharisha kwa motto.


Sababu ya kutapika kwa watoto.
 Kuna sababu ya uwezekano wa kutapika katika watoto, ambayo ni ilivyoelezwa hapo chini


  •  gastroenteritis
    Gastroenteritis ni maambukizi ya utumbo. Ni kitu cha kawaida inayosababisha kutapika kwa watoto na kwa kawaida huchukua muda wa siku chache .
  • maambukizo ya hatari
    Watoto wadogo hasawapo  katika hatari ya kupatwa na maambukizi kama vile pneumonia au maambukizi ya figo. Unapaswa kuwasiliana na daktari wako kama motto ana dalili ya magonjwa haya.
  • ugonjwa wa kidole tumbo
    Ugonjwa wa kidole tumbo










JINSI YA KUTENGENEZA MAZIWA YA CHUPA YA UNGA KWA MTOTO MCHANGA (FORMULA MILK)



Kinga hasili (immunity) ya kichanga chako sio imara kama ya mtu mzima, hivyo vichanga huweza kupata maambukizi ama malazi upesi kuliko mtu mzima. ii inamaanisha usafi ni muhimu sana sana wakati wa kumtengenezea kichanga chakula.

Vyombo vyote vinavyotumika kutengenezena chakula cha mtoto vinatakiwa viwe sterile (Yaani viwe kwenye hali ambayo haina wadudu). Hivyo basi chupa, chuchu ya chupa, mfuniko wa chupa na vyote vya kumwandalia mtoto vioshwe na kusterelize kila kabla ya kuvitumia kumlisha mtoto ili kupunguza chance ya mtoto kupata maambukizi ya magonjwa kama kuharisha.

Wadudu wa Bacteria kwenye maziwa ya unga 

Ingawa maziwa ya unga huwa yamefunikwa na kuzibwa kabisa (sealed), yanaweza pia kuwa na bacteria ndani kama Cronobacter sakazakii na mara chache huwa na salmonella. Ingawa case kama hizi hutokea mara chache lakini maambukizi yake ni ya hatari sana kwa kichanga na yanaweza sababisha mauti.


Bacterial huzaliana kwa upesi sana kwenye joto la kawaida la ndani ya nyumba (room temperature), hata kama maziwa yataachwa kwenye fridge bado hawatakufa na wataendelea kuzaliana ingawa baridi upunguza kasi ya kuzaliana.

Ili kupunguza maambukizi, ni vizuri kutengeneza maziwa mara moja pale tuu mtoto anapoyahitaji. k/a*ti
Tumia maji ya kunywa ya bomba yaliyochemshwa, Usitumie maji yalichemshwa zamani. Ukishachemsha maji yaache yapoe kwa mda wa dakika 30 na sio zaidi ndipo uyatumie kutengeneza maziwa. Hii itahakikisha kwamba joto la maji bado halipungui 70C. Maji katika joto hili litaua wadudu wa maambukizi kama bacteria. Kumbukuka kuacha maziwa yaendelee kupoa kabla ya kumpatia mtotot anywe.

Usitumie maji ya chupa ya dukani kutengeneza maziwa 

Maji ya kununua dukani hayashauriwi sababu kwanza sio sterile alafu pia yanaweza kuwa na kiasi kikubwa cha chumvi (Sodium) ama Salphate unles kiwe si zaidi ya 200mg. Ikiwa ni lazima utumie maji ya dukani basi hakikisha unayachemsha pia.

Matengenezo


  • Chemsha maji ya bomba (usitumie ambayo yamechemshwa zamani)
  • Yaache yapoe kwa dakika 30 tuu ili joto lisipungue chini ya 70C.
  • Safisha eneo unalotumia kutayariashia maziwa
  • Ni muimu sana kunawa mikono yako
  • Tumia sterelizer kusterelise chupa za mtoto, ama kama hauna chemsha vyupa vya maziwa.
  • Tafadhari hakikisha unapochemsha ama kusterelise vyupa hakikisha unaifungua chupa yote yaani unatoa vifunuko, chuchu na kuvichemsha vyote pamoja.
  • Weka chuchu na kifuniko vikiangalia juu na sehemu safi
  • Fuata maelekezo ya kwenye kopo la maziwa jinsi ya kutengeneza, angalia level ya maji, anza kujaza maji kwenye chupa kwanza wakati yakiwa bado yamoto kabla ya kumimina maziwa.
  • Unapojaza maziwa kwenye kijiko hakikisha kiasi hakiwi kama kimlima ( kiwe flat) tumia kisu kama inawezekana.
  • Changanya maziwa mpaka poda isionekane.
  • Yaache yapoe zaidi ili mtoto asiungue wakati akinyonya.
  • Test joto la maziwa kwa kumimina kido kwenye kiganja cha mkono.
  • Maziwa yakibaki baad ya kunyonya yamwage.
  • Tafadhari usitumie microwave kupasha moto maziwa yanaweza kumuunguza mtoto.












Sunday 9 November 2014

FUNGUS WAKATI WA MIMBA (Thrush)



Ni kawaida kabisa kutokwa na majimaji mazito (vaginal discharge) ukeni wakati ukiwa na ujazito.  Usiwe na wasiwasi kama majimaji haya ni myepesi na yana muonekano wa rangi ya maziwa.

Dalili za kuwa na fungus ukeni:

·         Majimaji yakiwa mazito, myeupe na rangi ya maziwa, na yanayoonekana kama cottage cheese, ama maziwa ya mgando, ama yaliyoharibika.
·         Kama unawashwa, na kusikia kuvimba kama vile umejikwaruza, na muonekano wa uwekundu sehemu ya ukeni.
·         Inauma wakati wa kujamiiana
·         Unasikia kuchomwachomwa wakati unakojoa

Je nilipataje thrush:

Maambukizi ya ukeni wakati wa mimba ni ya kawaida. Thrush husababishwa na fungus  (yeast) wanaoitwa candida albicans ambao wapo na huishi kwenye miili yetu bila kusababisha tatizo lolote. Wapo pia kwenye mfumo wa chakula na mara nyingi hawana madhara yoyote kwetu na wala hautojua kama wapo.
Huwa wanaleta tatizo pale tuu wakati fungus hawa na vijidudu vingine ndani na nje ya mwili vinapopungua ama kuongezeka kuliko kiasi kinachitakiwa.  Unaweza kupata thrush pale ambapo:
·         Unapokuwa mjamzito mabadiliko ya hormones  kwenye mwili  husababisha mwili uwe na sukari nyingi kuliko kiasi inayoitwa glycogen ambayo husababisha fungus kuzaliana kwa wingi (wanatumia glycogen kama chakula na hivyo kuwapatia nguvu ya kujiongeza idadi).
·         Unapotumia antibiotics, dawa hizi huua vijidudu mwilini ambapo pia huua vijidudu vizuri vinavyopigana na vile vibaya, hivyo basi balance ya vijidudu hivi inakuwa imebadilika na hiyo kusabaisha vile vibaya vizaliane kwa nguvu.
·         Kisukari (Diabetes): kama una ugonjwa wa kisukari ambacho huujakicontrol pia husababisha thrush.
·         Kama immune system yako ni dhoofu. Hii inaweza kutokana na pia na matibabu ya magonjwa kama sarakani (cancer) ama magojwa na HIV.
Ingawa thrush sio magonjwa ya zinaa, yanawezekana kuambukizwa kama partner wako amepata maambukizi haya, hivyo mnashauriwa wote wawili mpate matibabu kwa wakati moja.

Kama unafikiria una thrush, tafadhari mwone daktari.

Daktari atakupatia dawa, ingawa wanashauri kutotumia chochote kipindi cha mlongo wa kwanza wa mimba (miezi 3 ya mwanzo) .
Dawa zingine ni za kuweka ukeni (kidonge), unashauriwa kuweka usiku wakati umelala ili inyonywe vizuri wakati umelala. Thrush ni vigumu kupona upesi hivyo basi ni vyema umalize dozi utakayopewa na daktari.  Tafadhari usichukue dawa za vidonge ambayo utahitaji kumeza, bado haijajulikana kama vina madhara gani kwa mtoto.

Je nifanyeje

·         Wakati unapojiosha ukeni, usitumie sabuni osha na maji masafi (sio ya kisima) ikiwezekana jichemshia maji kidogo tuu(kuua vijidudu) kwa ajili ukeni. Na ikiwezekana jioshe mara moja kwa siku kwani kujisafisha sana ukeni unaondoa wale wadudu wanaohitajika kulinda uke (Good Flora microorganism).
·         Usitumie mafuta yatakayoirritate ngozi kama pedi za kunukia, deodorant za ukeni, na  sabuni zakunukia.
·         Kula maziwa mgando yasiyo na sukari, ama ingiza maziwa ya mgando ukeni.
·         Kama utatumia maziwa mgando, njia rahisi ya kuweka ukeni ni kwa kutumia tampoo, chovya tampoo kwenye maziwa mgando, dumbukiza tampoo ukeni, iache kwa muda wa lisaa limoja, alafu itoe.
·         Kupunguza kueneza thrush, basi jifute toka mbele kwenda nyuma kila baada ya kutumia choo.
·         Vaa chupi za cotton 100%
·         Wakati wa kujamiiana tumia kilainisho(lubricant) kupunguza maumivu kama una thrush.

Je thrush itamfikia mtoto tumboni

Hapana, mtoto amefunikwa na mfuko na hatadhurika.
Hata hivyo ni muhimu kupata matibabu kabla ya kujifungua, kwani mtoto anaweza kuambukizwa wakati akitokea ukeni.
Kama hii ikitokea basi utahitaji matibabu wewe na mtoto, mtoto mara nyingi anakuwa na utando mweupe kwenye ulimi.
Utagundua thrush huja na kuondoka wakati wa mimba, na huchukua mda mrefu kuitibu lakini sio kitu cha kuogopa sana.






Saturday 8 November 2014

Ugonjwa wa kifafa (seizures) kwa watoto


Kifafa mara nyingi husababishwa na uvujaji wa wave za kama za umeme (electrical discharge) kwenye ubongo ama husababishwa na hali ya kuzimia (baada ya kupunguka kwa msukumo wa damu ubongoni). Dalili (symptoms) zinaweza hutofautiana kulingana na sehemu ipi ya ubongo imehusika, lakini mara nyingi utasikia hali ya mwili kusisimka sio kwa kawaida, misuli kuvutika/kukaza yenyewe, na pia kupoteza fahamu.
Baadhi ya vifafa vingine huwa ni matokeo ya magojwa mengine mwilini, kama upungufu wa sukari kwenye damu, maambukizi, kuuumia kichwa(head injuries), ajari za barabarani au kuoverdose madawa ya kulevya.  Pia kifafa kinaweza sababishwa na uvimbe kwenye ubongo ama tatizo linguine la afya linaloathiri ubongo. Kifafa mara nyingi hutokea zaidi ya mara moja.

Watoto wa chini ya miaka 5 huwa wanapata hali ya kifafa pale joto lao la mwili linapozidi degree 38 (100.4° F (38° C) aina hii ya kifafa inaitwa  Febrile seizure. Hii inaogopesha kama mzazi lakini hii hali ni ya dakika chache tuu, mara chache husababisha matatizo makubwa, especially kama joto hili limesababishwa na maambukizi kama meningitis.

Kwa watoto chini ya miaka 5, kuhold pumzi inaweza sababisha hali ya kifafa (seizure). Kuna watoto wakati wanapokasirika huwa wanashikiria pumzi (hawavuti pumzi kwa sekunde chache) kabla tuu ya kuachia kilio kikubwa, kabla ya kupoteza fahamu kifafa kufuatia. Mara nyingi hali hii huisha yenyewe.

Watoto wa umri zaidi ya miaka 5 wachache huwa na hali hii lakini mara nyingi huwa inaisha baada ya sekunde chache.

Kama mtoto wako ana kifafa ufanyeje
Kama mtoto wako amepatwa na kifafa basi unashauriwa kumlaza chini sehemu ambayo ni salama, wanashauri umlaze upande wake wa kulia. Ondoa kitu chochote cha hatari ambacho kipo karibu, kama vyupa, sindano, mawe n.k. Kama ana cheni shongoni ivue ama kama nguo ipo shingoni ivue pia isimkabe.  Usijaribu kupanua mdomo wa mtoto anapokuwa na kifafa ama kuweka kitu mdomoni kwake, pia usijaribu kuzuia kuweweseka kwake.
Mara tuu kifafa kinapoisha basi mfariji mtoto, ni muhimu kwa watoto kubaki kulala chini mpaka hali hii iishe kabisa nay eye mwenyewe akitaka kuinuka.
Tafadhari mwite daktari pale ambapo kifafa kinaendelea zaidi ya dakika 5, pia kama mtoto ana vitu vifuatavyo:
       . anashindwa kupumua
       .ameumia kichwa
       .ana magonjwa ya moyo
       .hajawahi kupata kifafa zamani
       .kama amekunywa sumu ama ameoverdose dawa.

Baada ya kifafa, mtoto huonekana kuchoka, amechanganyikiwa, na anaweza kulala usingizi mzito sana (postictal period) hauhitaji kumwamsha mtoto as long as anapumua vizuri. Usijaribu kump chakula mpaka mtoto aamke na aonekane kuchangamka.

Baada ya kifafa mtaarifu daktari kuangalia tatizo lililosababisha hiyo hali ni nini.








Sunday 5 October 2014

Tatizo la Kutokulala kwa watoto wachanga

Watoto wengi wadogo huwa wanapata shida sana kutulia na kulala wakati wa usiku. Kwa watu wengine hili sio tatizo kwao na kama haikusumbui mtoto wako kwenda kulala muda ambao wewe unaenda kulala, basi sio shida. Lakini, kama wewe, ama mtoto wako anasumbuka na tatizo la kushindwa kulala usiku unaweza kujaribu kufanya yafuatayo:

Kila mtoto ni tofauti na fanya tuu kile unachoona kinafaa kwa mwanao.


Kama Mtoto wako hataki kwenda kitandani:

  • Amua saa ngapi ama mda gani unataka mtoto awe anaenda kitandani.
  • Kwa kuanza, mda wa mtoto kwenda kulala ukikaribia (ule mda anaolalaga kila siku) anza kumpeleka kulala dakika 20 kabla kwa siku ya kwanza, alafu siku ya pili mpeleke dakika 30 kabla, ya tatu iwe dakika 40 kabla na kuendelea kuongeza dakika 10 kila siku mpaka ifikie mda ule unaotaka wewe.
  • Jipangie kikomo cha kukaaa na mwanao kitandani wakati wa kulala, mfano msomee hadithi moja tuu, alafu sema usiku mwema, muage na kumwacha alale.
  • Mpatie mtoto wako toy yake anayoipenda alale nayo, mfano kama huwa anatumia dummy ya mdomoni, ama kitaulo (kuna watoto hunyonya kitaulo) ama chochote kitakachombembeleza kulala. 
  • Kama mtoto wako analia, umwache kitandani na uondoke chumbani na mpatie dakika 5 mpaka 10 ya kujituliza mwenyewe kabla ya kumyamazisha tena.
  • Usimnyanyue ama kumbeba mtoto, ama kumtoa kitandani na kama mtoto atainuka na kutoka kitandani basi mchukue na kumrudisha kitandani tena.
  • Washa taa yenye mwanga mdogo (kama unayo) ama acha mwanga wa mbalamwezi uingie kama kutakuwa na ulazima huo.
  • Hakikisha amelala kabla ya kwenda kumwangalia mtoto ili usimwamshe tena.
  • Fanya hivi kila siku na usikate tamaa baada ya siku moja tuu, jipatie siku 5 ili mtoto awe na mazoea.

Kama mtoto anaamka mara kwa mara usiku.

 Ni kawaida kwa watoto wa zaidi ya miezi 6 kulala usiku mzima bila kuamka, Hata hivy, kuna watoto wengi  chini ya miaka mitano huwa hawalali usiku mzima bila kuamka. Kuna ambao watarudi kulala tena wao wenyewe na wengine ambao watalia kwa kutaka uwepo wa mtu.

Kama hii hali itatokea, jaribu kutatua tatizo linalimfanya mwanao aamke usiku.
Je ni njaa? kama mwanao ni mkubwa zaidi ya mwaka moja, maziwa na uji huwa yanaweza mfanya alale usiku mzima kama hivyo ndio alikunywa mda tuu kabla ya kulala.

Je ni uoga/hofu ya giza? unaweza kutumia taa za usiku ama unaweza acha taa ya corrido iwake usiku.

Je ni ndoto mbaya? kama ni hivyo jaribu kutafuta kama kuna kitu kinachowasumbua ambacho ndio husababisha kuota usiku.

Je ni joto/ baridi kali? kama ni hivyo punguza ama uongeze nguo za kujifunika ama punguza/ongeza joto ama baridi kwenye chumba kwa kufungua milango ama kupunguza AC.



Kama hakuna sababu maalumu inayomfanya mwanao aamke, alie ama kutaka ukae nae usiku basi jaribu yafuatayo:

  • Mda wa kuamka - kama mwanao huamka wakati huo huo kila usiku basi jaribu kumwamsha kati ya dakika 15 mpaka 60 kabla alafu mbembeleze tena kurudi kulala. 
  • Mruhusu mtoto alale chumba kimoja na kaka yake ama dada yake kama tatizo ni kuogopa kuwa peke yake. Hii itawasaidia wote walale usiku mzima.
  • Mfundishe mwanao kujirudisha kulala yeye mwenyewe usiku, kwanza kama kila kitu kiko sawa, mmbembeleze mwanao kulala bila ya kuongea nae sana akiwa kitandani. Kama anataka kinywaji mpe maji ila angalisho usimpatie chakula wakati akiwa ameshtushwa na usingizi. Ili njia hii ifanye kazi ni lazima  umwache mtoto kitandani na usimnyanyue na kwenda nae sebuleni, ama chumbani kwako. Mwache alie kwa kati ya dakika 5 hadi 10 ndipo ukamwangalie tena. Mwambie arudi kulala na mwakikishie kwamba hakuna kitu cha kuogopesha na usiongee nae kitu kingine, kama ni mtoto mchanga mbembeleze kwa kumpapasa mgongoni akiendelea kulia mbebe kwa dakika 2 tuu alafu mrudishe kitandani.  mwache kama analia ikifika dakika 10 nenda tena, fanya kama hapo juu na umwache ena ajirudishe kulala. Endelea hivyo kwa siku kadhaa na mtoto atazoea na kuanza kusinzia mwenyewe ukimweka kitandani. 
  • Msaidiane na mumeo, mnaweza mkafanya zamu ya kumwangalia mtoto anapolia, hii pia husaidi mtoto kuwajua na kuwazoea wazazi wote wawili, pia itamfanya mama asichoke sana.

Ndoto za kutisha



Ndoto za kutisha ni kawaida kabisa. Wao mara nyingi huanza kati ya umri wa miezi 18 na miaka mitatu. Ndoto hizi ni si kawaida ni ishara ya masumbuko ya hisia. Huwa inaweza kutokea kama mtoto wako ana wasiwasi juu ya kitu au amepata hofu na kipindi ama hadithi aliyoangalia kwenye luninga.  Baada ya ndoto, mtoto wako atahitaji faraja na uhakika. Kama mtoto wako anaota ndoto hizi sana na hujui ni kwa nini basi ongea na daktari.
 
Kuweweseka usiku

Hutokea kabla ya umri wa mwaka moja ingawa pia ni kawaida zaidi kwa watoto kati ya umri wa miaka mitatu hadi nane. mara nyingi mtoto huweweseka na kupiga kelele ama kupigapiga mikono na miguu akiwa bado yupo usingizini. hutokea baada masaa machache ya kulala, wanaweza kukaa na kuongeaongea wakiwa usingizini na kuonekana wenye hofu wakiwa usingizini. Wala usiogope na mtoto wako itafika wakati itapita tuu.

Usimwamshe mwanao wakati akiweweseka ila kama hutokea mda huohuo kila usiku basi jaribu kumwamsha dakika 15 kabla ya muda ule anaoweweseka kila siku. abaki macho kwa dakika chache kabla ya kumrudisha kulala tena.



I hope hayo maelezo hapo juu yamesaidia, pia angalia mtoto kutokulala usiku







Tuesday 30 September 2014

Ugonjwa wa vipele kutokana na nappy za kutupa (mapampas)

Leo nimeona tujulishane na kubadilishana mawazo kuhusu hili suala la allergy ya diapers (tunayaita mapapas) kwa watoto wetu. Kutokana na mabadiliko ya kimaendeleo siku hizi sio kama zamani watotot wetu yumezowea kuwavalisha chupi/ nappy za kutupa, yaani zikishajaa mikojo hatufui tena badala yake unazitupa.

Vipele kutokana na diapers ni kawaida kwa watoto na sio ishara ya kumtelekeza mtoto. Huu ni ugonjwa wa ngozi amba unatokana na kugusana na kitu ambacho husababisha allergy na matokeo yake vipele hutokea. Angalia picha zifuatazo:

Huu ugonjwa husababishwa na bacteria ama fangasi ambao kwa kawaida huwepo kwenye ngozi ya mtoto.

Kumbadilish mtoto diaper mara kwa mara inasaidia kupunguza vichochezi kwa allergy hii.  Vichochezi huwepo kwenye ngozi ya mtoto.

Mtoto anapokuwa na ugonjwa huu jitahidi kuacha kutumia baadhi ya mafuta ama creams ambazo zisizopitisha hewa kuingia kwenye ngozi (mfano, petrolium jelly, mafuta ya mgando ya kupaka) na wakati mwingine antifungal cream, low-potency hydrocortisone cream. High-potency steroid creams, powders, na baking-soda/boric-acid baths and neomycin-containing ointmentspia ni za kuziepuka.












 Nini husababisha vipele vya diaper

Kuna makundi kadhaa ya sababu wa ugonjwa huu wa ngozi Kwanza kabisa ni "kikereketa" au "kugusana(contact)"  Ngozi huonekana nyekundu (kama vile imechomwa na jua) alafu hubadilika na kuwa na tabaka (layer) juu wa ngozi. Tofauti ya ugojwa huu na magonjwa mengine ya ngozi ni kwamba utagundua kutokuwepo kwa vipele sehemu zenye mikunjo kwenye ngozi ya mtoto (matakoni), hii inaonyesha kwamba mkojo na kinyesi huchangia kwani mikojo na kinyesi huwa na wadudud wa bacteria na fungus. Mikojo na kinyesi huwa hazifiki sehemu zenye mikunjo na ndio maana hakuna wadudu hawa, hivyo vipele huwa havionekani sehemu hizi

Bacteria aina ya (Staph na Strep) na fungus aina ya candida mara nyingi ndio huonekana kwenye ugonjwa wa diaper. Kama imesababishwa na bacteria basi huanza kwa kusababisha vipele vidogodogo (Impetigo) ambavyo huja kuwa malengelenge na kupasuka na kujisambaza, matakoni na sehemu za karibu,  hii husababisha  kuwashwa kwa ngozi.

Kama imesababishwa na fungus basi huoneka ngozi madoa madoa  myekundu na ukubwa (kati ya 2mm - 4mm). Mara nyingi huonekana karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa. 

Ugonjwa huu ni rahisi kuujua kwa macho tuu, ukiwa na tatizo mpeleke mtoto kwa daktari. 

Vikereketa mara nyingi hutokana na harufu na material ya diaper. Ingawa ni mara chache sana allergy ndio sababu ya ugonjwa huu, lakini kama ukiona tatizo ni diaper basi badilisha diper. Pia ikiwezekana jaribu kutumia wipes zisizo na harufu.

Tufanyeje?


Dawa kubwa ni kuzuia mtoto asipate huu ugonjwa, nimelist vitu vya kufanya kama ifuatavyi:

1. Wewe kama mzazi (mama ama baba) unatakiwa kumkagua mtoto kila siku, nasema hivi sababu wazazi wengi huwaachia mabinti wa kazi kulea mtoto na  hujisahau majukumu yao kama wazazi. Hi itasaidia kuona kama ugonjwa huu unapoanza.

2. Jitahidi kumuogesha mtoto asubuhi na kabla hajaenda kulala, hii mara nyingi husaidia safisha kikereketa ambacho kilibaki kwenye diaper (ikiwezekana msafishe mtoto na maji kila unapombadilisha diaper badala ya kutumia wipes) Wipes zitumike pale ambapo maji hakuna.

3. Upele unapotokea, msafishe na maji na nguo safi na laini na sio wipes. 


Kwa maelezo zaidi tembelea zifuatazo

Hapa na hapa 




















Tuesday 17 June 2014

Ugonjwa wa vipele vya nappy kwa watoto

Vipele vya nappy ni ugonjwa wa kawaida kwa watoto, huwa vnasababishwa baada ya ngozi ya mtoto napokutana na mkojo ama mavi ambayo yanabebwa na nappy.

Vipele hivi hufanya ngozi ya matakoni ya mtoto kuvimba, ngozi ya matakoni  huwa imezungukwa na vipele. Ikitokea hivi utahitaji kumbadilisha nappy mara kwa mara.

Vipele hivi zinaweza kutibiwa kwa cream unaweza ipata toka pharmacy. Unaweza kuacha kutumia wipes mpaka vipele vitakapopona kabisa.