MIMBA WIKI YA 5 NA 6

MTOTO
 Mtoto ndo kwanza ana ukubwa kama mbegu ya chungwa kama 5mm hivi.  Central nervous system, Ubongo na uti wa mgongo tayari vimeshaanza kujengwa na vimeanza kukua. Miguu na mikono nayo imeanza kutengenezwa pamoja na uso pia
.


MWILI WAKO
Unaweza kuona matone ya damu kidogo yakitoka, hii ni kawaida ilimradi yawe na rangi iliyofifia. Hii inatokana na yai la mimba kujikalisha vizuri kwenye uzazi na mara nyingi haya hutokea kipindi ungetegemea kuona udhi.
Hatahivyo, kama utaona damu kipindi chochote wakati wa mimba ni muhimu kwenda kumuona daktari wako kuhakikisha kama hakuna tatizo na mtoto.

Maziwa utayahisi yako tender (yanavimba na kuuma kwa mbali ukiyabinya). Hii inatokana na kuongezeka kwa hormone mwilini ambazo husababisha kuandaa maziwa kujitengeneza tayari kwa ajili ya mtoto atakapozaliwa. Mara nyingi uvimbe na maumivu yanapungua kidogo mwishoni mwa mlongo wa kwanza wa ujauzito.
Mwili utasikia uchovu wa ajabu, usishangae ingawa ni ngumu kuvumilia, ukichukulia kwamba labda haupo tayari kuwaambia watu kwamba una mimba. Pumzika kila uwezapo kipindi hiki kitaisha soon.

Kama unakunywa pombe unashauriwa kuacha, pia uache kuvuta sigara kwani yana madhara kwa mtoto

Endelea kutumia condomu (Mipira) kwani kama mpenzi wako ana ugonjwa wa zinaa atamuambukiza mtoto pia.