Kifafa mara
nyingi husababishwa na uvujaji wa wave za kama za umeme (electrical discharge)
kwenye ubongo ama husababishwa na hali ya kuzimia (baada ya kupunguka kwa
msukumo wa damu ubongoni). Dalili (symptoms) zinaweza hutofautiana kulingana na
sehemu ipi ya ubongo imehusika, lakini mara nyingi utasikia hali ya mwili
kusisimka sio kwa kawaida, misuli kuvutika/kukaza yenyewe, na pia kupoteza
fahamu.
Baadhi ya
vifafa vingine huwa ni matokeo ya magojwa mengine mwilini, kama upungufu wa
sukari kwenye damu, maambukizi, kuuumia kichwa(head injuries), ajari za
barabarani au kuoverdose madawa ya kulevya. Pia kifafa kinaweza sababishwa na uvimbe
kwenye ubongo ama tatizo linguine la afya linaloathiri ubongo. Kifafa mara
nyingi hutokea zaidi ya mara moja.
Watoto wa chini ya miaka 5 huwa wanapata hali ya kifafa pale
joto lao la mwili linapozidi degree 38 (100.4° F (38° C) aina hii ya kifafa inaitwa Febrile seizure. Hii inaogopesha kama mzazi
lakini hii hali ni ya dakika chache tuu, mara chache husababisha matatizo
makubwa, especially kama joto hili limesababishwa na maambukizi kama
meningitis.
Kwa watoto chini ya miaka 5, kuhold pumzi inaweza sababisha hali ya
kifafa (seizure). Kuna watoto wakati wanapokasirika huwa wanashikiria pumzi
(hawavuti pumzi kwa sekunde chache) kabla tuu ya kuachia kilio kikubwa, kabla
ya kupoteza fahamu kifafa kufuatia. Mara nyingi hali hii huisha yenyewe.
Watoto wa umri zaidi ya miaka 5 wachache huwa na hali hii lakini mara
nyingi huwa inaisha baada ya sekunde chache.
Kama mtoto wako ana kifafa ufanyeje
Kama mtoto wako amepatwa na kifafa basi unashauriwa kumlaza chini sehemu
ambayo ni salama, wanashauri umlaze upande wake wa kulia. Ondoa kitu chochote
cha hatari ambacho kipo karibu, kama vyupa, sindano, mawe n.k. Kama ana cheni
shongoni ivue ama kama nguo ipo shingoni ivue pia isimkabe. Usijaribu kupanua mdomo wa mtoto anapokuwa na
kifafa ama kuweka kitu mdomoni kwake, pia usijaribu kuzuia kuweweseka kwake.
Mara tuu kifafa kinapoisha basi mfariji mtoto, ni muhimu kwa watoto
kubaki kulala chini mpaka hali hii iishe kabisa nay eye mwenyewe akitaka
kuinuka.
Tafadhari mwite daktari pale ambapo kifafa kinaendelea zaidi ya dakika
5, pia kama mtoto ana vitu vifuatavyo:
. anashindwa kupumua
.ameumia kichwa
.ana magonjwa ya moyo
.hajawahi kupata kifafa
zamani
.kama amekunywa sumu ama
ameoverdose dawa.
Baada ya kifafa, mtoto huonekana kuchoka, amechanganyikiwa, na anaweza kulala
usingizi mzito sana (postictal period) hauhitaji kumwamsha mtoto as long as
anapumua vizuri. Usijaribu kump chakula mpaka mtoto aamke na aonekane
kuchangamka.
Baada ya kifafa mtaarifu daktari kuangalia tatizo lililosababisha hiyo
hali ni nini.
No comments:
Post a Comment