Tuesday, 17 June 2014

Ugonjwa wa ngozi watoto


Contact demartitis ni  ugonjwa wa uvimbe wa ngozi ambao hutokea wakati  unapogusa kitu .

Huu ni ugonjwa wa aina ya eczema ambayo unaweza kusababisha ngozi kuwasha na kuwa na magamba, wakati mwingine kuhisi kuungua na kuchoma. Husababisha ngozi kuwa na mapele yenye maji ambayo huchubuka, kuwa kavu na kupasuka.







Inaweza kuathiri sehemu yoyote ya mwili lakini kwa kawaida huathiri mikono.

Kusoma zaidi juu ya dalili za ugonjwa huu bonyeza http://www.nhs.uk/Conditions/Eczema-%28contact-dermatitis%29/Pages/Symptoms.aspx

Ugonjwa huu husababishwa na:

  •      kikereketa (Kitu kinachosababisha kidonda kwenye ngozi), au
  •      allergen (Kitu kinachosababisha mfumo wa kinga mwilini kupigana matokeo yake     huathiri ngozi) 



Kutibu Contact Dermatitis

Kama unaweza kufanikiwa  kuepuka kikereketa (irrritants) au allergener zinazosababisha contact dermatitis basi hali yako itapona.

Hata hivyo, hii haiwezekani wakati wote, hivyo matibabu ya kutumia emollients yanahitajika.  Imollients ni mafuta yanayosaidia kutopotea kwa maji ngozini.  Madawa ya steroidi yanaweza kutumika kutibu dalili kali.

Baada ya matibabu, watu wengi wenye ugonjwa huu hupata nafuu na hatimaye kupona. Hata hivyo, baadhi ya watu wanaweza kupata matatizo, dalili kali ambayo kuathiri ubora wa maisha yao.

 


Tuesday, 11 June 2013

Mtoto miezi 6 mpaka 12


Rudi mtoto chini ya miezi 6

Mtoto miezi 6 mpaka 12

Mpaka wa 6, mtoto anaweza kulala muda wa masaa 3 wakati wa mchana na kulala zaidi ya masaa 9 hadi 11 wakati wa usiku. Katika umri huu, unaweza kumuacha alie usiku, hii ni kwa watoto wachanga ambao huamka na kulia wakati wa usiku.

Wazazi wanaweza kuwapatia watoto muda kidogo watulie na kujirudisha kulala wao wenyewe bila kubembelezwa. Kama huwezi kumwacha mwanao akilia basi mbembeleze bila kumbeba kwa kumuongelesha akiwa kitandani huku unamsugua (rub) mgongoni kidogokidogo, alafu muache uondoke akijua kwamba anatakiwa kurudi kulala - isipokuwa kama anonekana kuwa mgonjwa. Watoto wagonjwa wana haja ya kubebwa na kutunzwa. Kama mtoto wako haionekani mgonjwa na anaendelea kulia, unaweza kusubiri kwa muda mrefu kidogo, kisha rudia tena kumwacha ajibembeleze yeye mwenyewe atakapolia tena.

Kati ya miezi 6 na 12, wasiwasi wa kutengana toka kwa mama humpata mtoto, hii ni kawaida na ni sehemu ya ukuaji ya mtoto. Sheria ni ileile, jaribu kutombeba mtoto wako, kutomwashia taa, kutomwimbia, kutomwongelesha, kutocheza nae, au kulisha mtoto wako wakati anatakiwa alale. Hizi zote hazitamruhusu mtoto wako kujifunza kulala mwenyewe na ataendelea kuamka usiku.

Watoto chini ya miaka 3
Kuanzia mwaka 1 hadi 3, wengi wachanga kulala masaa 10 hadi 13. Kujitenga wasiwasi, au tu hamu ya kuwa pembeni na mama na baba (ili asimiss kitu), inaweza kuwahamasisha mtoto kukaa macho.

Wazazi wakati mwingine kufanya makosa ya kufikiri kwamba kumwacha mtoto asilale mapema kutamfanya mtoto alale zaidi usiku. Kiukweli, ingawa, watoto wanaweza kuwa na wakati mgumu kulala kama wamechoka sana. Ingawa watoto hulala kidogo mchana, usimlazimishe alale mchana kama hataki, lakini ni muhimu kuwa na ratiba ya muda wa utulivu kwa mtoto, akae chumbani kwa mda hata kama kataki kulala mchana.

Kuanzisha utaratibu wa kwenda kulala husaidia watoto kupumzika na kuwa tayari kwa ajili ya usingizi. Kwa mtoto, utaratibu unaweza kuwa toka dakika 15 hadi 30 na ni pamoja na shughuli za kutulia kama vile kusoma hadithi, kuoga, na kusikiliza muziki laini.

Chochote utakachofanya, mwanao anatakiwa ajue ni usiku na anatakiwa alale, usibadilishe mpangilio ulouweka kila siku kabla ya kulala.  Kila inapowezekana, mruhusu mwanao achague nini anataka usiku huo, yaani kama ni hadithi, ama kuimbiwa, nguo  gani ya kulalia anataka, toy ipi ya kulala nayo anataka, nyimbo iipi, hadithi ipi n,k ilimradi bado mtafuata mpangilio uleule kila siku. Hii inamfanya anaona ana udhibiti kwenye huu mpangilio.

Lakini hata mtoto mlalaji  huwa anaamka mara moja moja. Kuota meno kunaweza  kumuamsha pia ndoto. Ndoto huanza katika umri huu, na kwa watoto wadogo, ndoto inaweza kuwa ni kutisha. Jinamizi ni hasa inatisha kwa watoto, ambao hawawezi kutofautisha mawazo na ukweli. (Basi kuwa makini kuchagua programu gani mwanao anaangalia  kabla ya kwenda kulala)


Kuwafariji na kushikilia mtoto wako kwa nyakati hizi. Kuwa na majadiliano juu ya ndoto kama yeye anataka, na kukaa hadi mtoto wako ni atulie. Kisha muhimize mtoto wako arudi kulala mapema iwezekanavyo.

Mtoto kutolala usiku

Je mwanao huwa ana tabia ya kuamka usiku? 
Huwa anakufuata chumbani kwako?
Anataka kulala pembeni yako?

Watoto wanapokuwa wachanga huwa wananyonya maziwa ya mama ama ya chupa kila baada ya masaa machache. Hivyo mazoea ya kuamka usiku kwa ajili ya kunyonya huwa yanaendelea pindi mtoto huyo anapokuwa na umri wa kuweza kulala usiku bila kutegemea chakula. Hii huwa inatokana na mzazi/wazazi kuiendeleza iyo tabia kwa kumpatia mtoto maziwa usiku. mtoto pindi anapoanza kuanza kula chakula kigumu         basi unaweza kuanza kumtoa kwenye kunyonya usiku polepole mpaka ataweza kulala mwenyewe usiku mzima bila kuamka.

Kama unataka kurekebisha hiyo tabia unaweza kufanya yafuatayo:

Kiasi gani cha usingizi kinatosha kwa mwanao?

hii inategemea na umri wa mtoto na mtoto mwenyewe. Watoto wapo tofauti, Hermes anaweza kulala toka saa 2.00 usku mpaka saa 2 asubuhi, wakati Henrick yeye ni mtoto wa maluelue analala atalala kuanzia saa 3 usiku na kuamka saa 12 asubuhi. utamjua mwanao kama ana usingizi/anakosa usingizi mara tabia zake zikichange, anaweza kuwa juu juu, mbishi na analialia.  hizi chini ni masaa ya kulala kwa mtoto kutegemeana na umri wake:

Watoto chini ya miezi 6

Hakuna formula ya kulala kwa ajili ya watoto wachanga  kwa sababu saa zao mwilini hazijakamilka bado. Wao kwa ujumla huwa wanalala au drowse kwa masaa 16 hadi 20 kwa siku, hii ni kati ya usiku na mchana.

Watoto wachanga lazima waamshwe kila baada ya masaa 3 na 4 hadi uzito wao uwe imara, ambapo kwa kawaida hutokea ndani ya kipindi cha wiki moja. Baada ya hapo ni sawa kama mtoto akilala kwa muda mrefu zaidi.
Baada ya wiki chache za mwanzo, watoto wachanga wanaweza kulala kwa muda mrefu kama masaa 4 au 5  huu ndio muda ambao matumbo yao madogo yanaweza kumudu kati ya ulishaji. Kama watoto hulala vizuri wakati wa usiku, basi watakula zaidi wakati wa mchana.

Wakati tu wazazi wanapohisi kuwa kulala usiku kunaonekana kama ndoto ya mbali, usingizi wa mtoto wao kawaida huanza kuhama kuelekea usiku. Anapokuwa na miezi 3, mtoto hulala kwa wastani wa masaa 13 katika kipindi cha saa 24 (yale masaa 4-5 ya kulala wakati wa mchana  huvunjwa katika kulala mara mojamoja(naps) na masaa 8-9 wakati wa usiku. Asilmia 90% ya watoto wa umri huu hulala usiku mzima, kwa maana ya masaa 5 hadi 6 katika mfululizo.

Lakini ni muhimu kutambua kuwa watoto hawawi macho saa zote, wakati wanasikika kama wapo macho, wao wanaweza kulia na kufanya kila aina ya kelele nyingine wakati wa usingizi wa mang'amung'amu. Hata kama wakiamka usiku, wanaweza tu kuwa macho kwa dakika chache kabla ya kurudi tena kulala wao wenyewe bila kubembelezwa. 

Kama mtoto chini ya umri wa miezi 6 anaendelea kulia, ni vizuri kwenda kumsikiliza. Mtoto wako inawezekana kuna kitu kinachomfanya alie, njaa, joto, amekojoa, baridi, au hata mgonjwa. Lakini mara kwa mara usiku kumuhudumia mtoto usiku kwa ajili ya kumbadilisha na kumlisha lazima iwe ya haraka na kimyakimya. Kipindi hiki usifanye chochote kile kitakachomwamsha mtoto kama kuzungumza, kucheza, au kuwasha taa. Muhimiza kwamba ni usiku na ni kwa ajili ya kulala. Unamfundisha hili kwa sababu mtoto wako hajali ni muda gani ilimradi mahitaji yake yanakamilishwa.

Kimsingi, mtoto wako lazima awekwa kwenye kitanda kabla ya kuanza kusinzia. Na si mapema mno kuanzisha kamchezo cha kwenda kulala mda fulani kila siku, unaweza kumzoesha kumwimbia kabla ya kilala, fanya mfululizo na katika utaratibu huo kila usiku.

Lengo ni kuwafanya watoto walale kwa kujitegemea, na kujifunza kujibembeleza wenyewe na kurudi kulala pindi wanapoamka usiku wa manane.

Angalia mtoto miezi 6 mpaka 12







Tuesday, 16 April 2013

Unawezaje kupata mtoto wa kike?



Haya wanduguuu, wataalamu wanasema kwamba huwezi kuamua ni mtoto gani unayemtaka kabla ya kuconceive. Hii inatokana na kwamba hujui kama kwenye mbegu ya kiume ni chromosome X ama chromosome Y ndio iliogelea kwa kasi zaidi kuliko yenzake. Mimi binafsi nina vidume viwili na ningependa kweliii nipate wa kike. Hivyo basi nimeamua ku-dig nikapata mawili matatu, eti wanasema kuna njia (Ambazo nitajaribu) ambazo zinaweza kumsaidia X awe mjanja ama Y kuwa mjanja. Lakini kwa leo nitagusia jinsi gani ya kumsaidia X kuwa mjanja.

Mbegu ya mwanaume ina chromosomes mbili, Y na X, mbegu hii ina kiwango sawa cha X na Y (50/50). Y inapo-conceive ndipo unakuwa na mtoto wa kiume na X inaposhinda unapata mtoto wa kike. Ingawa Y anaonekana mjanja na mwepesi kuliko X, haina nguvu kama X. Kujua hili inasaidia kupanga jinsi ya kumpata mtoto wa kike, hii ndio silaha yako.  Y kutokuwa na nguvu kunamaanisha kwamba Y anakufa upesi kuliko X, hivyo basi fanya ufanyavyo kuhakikisha kwamba Y anakufa ili ubakiwe na X tuu.

Pangilia mda mzuri wa kupata mtoto wa kike: Y-chromosome ina haraka lakini haiishi zaidi ya siku tatu na X chromosome haina haraka lakini huishi mpaka siku tano. Hivyo basi jaribu ku-conceive siku tatu kabla ya ovulation yako ianze. Ila, ukishafanya mapenzi hiyo siku ya tatu kabla ya ovulation kuanza hutakiwi kufanya tena mpaka ovulation iishe. Hii inatokana na sababu ifuatayo: Unapofanya mapenzi siku tatu kabla ya ovulation, zile mbegu za kiume zenye X na Y zinaanza kuogelea na kupigania kwenda kwenye yai la mwanamke lakini mbegu ya mwanamme haito-conceive sababu ovulation kwa mama inaanza baada ya siku tatu, yaani mbegu za mwanamme zimeingia mapema (During the safe days) kabla ya ovulation. Kwa sababu Y chromosome haiishi zaidi ya siku tatu, basi siku ya tatu pindi ovulation kwa mama inapoanza tayari Y chromosome zitakuwa zimeshakufa na mbegu za mwanaume zitakuwa imebakiwa na X chromosomes tuu. Hivyo basi unajipatia chance kubwa ya kuwa na mtoto wa kike.

Ili hii plan ifanye kazi, unatakiwa uwe na uhakika siku yako unapoanza ovulation (yaani kipindi unachoweza kushika mimba). Labda umeshasikia kwamba ovulation inaweza anza kuanzia siku ya 14 ya mzunguko wako ingawa hii inatofautiana tofautiana. Kuna njia nyingi ya kujua lini unaovulate, dalili za kuonyesha ovulation angalaia hapa. Kuna vifaa ambavyo vinasaidia ku-predict ovulation yako, vinaitwa "Ovulation test kits", vinavyotumia saliva ni vizuri zaidi kuliko za mkojo kwani unaweza kurudia kutumia mara nyingine.

10 x Ovulation Test Kits  Accurate Ovulation Prediction Test Cassettes Muonekano wa Ovulation kits

Position wakati wa mapenzi:

Jaribu kufanya mapenzi kwenye position ambayo ni vigumu kwa mbegu za kiume kujipenyeza ndani, hii ili kuzipatia kazi ngumu ya kulifikia yai la kike. Positions hizi ni kama zifuatazo:

 Spooning Position:                                           Traditionary missionary position



                               

                          
PH ya mwili:  Mwili ukiwa na acid nyingi inasaidia kuua chromosome Y upesi. Kama nilivyosema hapo mwanzo Y haina nguvu, hivyo kwenye mazingira ya acid inakufa upesi. Hivyo basi unashauliwa kula vyakula vyenye kiasi kikubwa cha acid. Vyakula hivi ni kama: apples, blueberries, cherries, grapes, grapefruit, nectarines, peaches, pears, pineapple, plums, raspberries. Kuna recipe ya kukupatia acid nyingi mwilini kama hivi. Pia kuna njia nyingine ya kuongeza mazingira ya acid kwenye sehemu ya mwanamke, hii ni kuyakalia maji ya acid (kama maji ya vinegal) kabla ya kufanya mapenzi. 

Kwa ufupi tuu, ukichanganya njia zote tatu utakuwa na chance kubwa ya kupata mtoto wa kike (90%).

Nitawajulisha kama nitafanikiwa, all the best my dears na good luck kwa kutafuta mtoto wa kike.
                           







PH ya mwili




Wednesday, 24 October 2012

Mimba wiki ya 7 na 8

Mtoto

Mtoto tumboni anaendelea kukua  na ni mara 10000 kwa ukubwa kuliko alivyokuwa kipindi mimba inatunga. Kiasi kikubwa cha ukuaji ni ujengaji wa kichwa cha mtoto kwani sasa celli mpya za ubongo zinatengenezwa. mdomo na ulimi vinatengenezwa pamoja na miguu na mikono na maini yanajiandaa kufanya kazi yake pia.

Mwili wako

Unapofikia hapa kifua kinakuwa kimeshaongezeka kwa ukubwa, hormones zimeongezeka ka kasi kali na utakuwa umeshaongezeka kwa unene pia.
Chakula bado utakiona kibaya na hata unaweza tapika ukisikia Harufu ya chakula. Jaribu kula chakula ambacho hakikuchefui kwa kipindi hiki.
Pia utatumia muda wako mwingi chooni siku hizi, Hormone inayoitwa hCG inaongeza upitishaji wa damu maeneo ya pelvis (kwa wale wanaopenda fanya mapenzi, huu ndo wakati muafaka) na hii husababisha kutaka kwenda choo ndogo mara kwa mara. Bado unahitaji kunywa maji/juice nyingi sana kwani wote wawili mnahitaji kimiminika mwilini.  Watu wengi huwa wanajisikia vibaya kwa sababu ya kuishiwa na damu ama maji mwilini, hii hali inasabisha wajisikie kuzimia na kuanguka. Pia sijui kama ni kweli, eti wanasema kama unaumwa sana kipindi cha mlongo wa kwanza basi mtoto ni wa kike, hii inatokana na hormone za kike za mama pamoja na za mtoto wa kike tumboni zinakuwa nyingi zaidi kuliko kama ungekuwa na mtoto wa kiume, kwani mtoto wa kiume hatoi hormone hizo kwa wingi.
Uchovu ni kitu kingine cha kuwa makini nacho, kula chakula kidogokidogo mara kwa mara inasaidia kukupatia nguvu mwilini. 

Pia unaweza kuwa na mate mengi mdomoni, hii ni kwa mlongo wa kwanza tuu lakini ni ya kupita tuu, jaribu kula chewing gum zisizo na sukari zinaweza saidia.

Kiungulia ni tatizo jingine unaloweza kupata kipindi hiki, jaribu kutokula chakula chenye spicy nyingi kama pilipili, chakula cha fat nyingi, chakula cha cafeine kama kahawa. Pia, jaribu kutokumywa maji kabla/mara tuu ya kula chakula kwani mchanganyiko wa maji na chakula tumboni unasababisha kiungulia.

Ukosaji wa choo ni tatizo jingine kipindi hiki, mimba inasababisha mishipa kwanye sehemu ya choo kikubwa i-relax na kuruhusu kinyesi kibaki tumboni kwa mda mrefu, hivyo hujikusanya kwa wingi na siku utakapopata choo kinakuwa ni kigumu sana.maziwa mgando na papai lililoiva sana vinaweza saidia.


Wednesday, 8 June 2011

Mimba Wiki ya 3 na ya 4

Mwili wako

Hongera, inawezekana bado hujui lakini una mimba. Ingawa hauhisi chochote bado mwili wako tayari unafanya kazi kwa kasi kujiandaa kwa ajili ya miezi tisa ijayo.

Nini Kinafanyika ndani ya kizazi(Uterus)

Kizazi kawaida kina uzito wa 60g na 7.5cm kwa urefu, Lakini pindi tuu uzazi unapotunga kinaongezeka kwa ajili ya uongezefu wa hormone inayoitwa oestrogen ambayo inatolewa na placenta. Hormone hii ni muhimu kwani ndio inayo saidia kutengenezwa na kukuza kwa mtoto tumboni, viungo kama mapafu, maini, kidney n.k havitakomaa pasipo hii hormone. Uzazi unanenepa na kusababisha layer kubwa ya majimaji ambayo ndipo mtoto atakapoishi na kukua kwa kipindi chote cha ujauzito. kipindi hichohicho muscle fibers zinajijenga kujiandaa kuzaliwa kwa mtoto.


Nini kinafanyika kwenye shingo ya uzazi (Cervix)

Shingo inaongezeka kidogo kwa upana, inarainika na rangi yake kuwa nyeusi zaidi kuliko kawaida sababu ya kuongezeka kwa uwingi wa mishipa ya damu kwenye eneo hilo. Glands kwenye cervix inajenga ute mzito (Mucus plug) kugundisha shingo ya kizazi ili kisipatwe na maradhi kumkinga mtoto akiwa tumboni.

Kwa kipidi hichi chote hautoona hedhi mpaka ujifungue.

Thursday, 2 September 2010

Ujauzito

Hongera, baada ya kuona dalili za mimba sasa unaingia mlongo wa kwanza wa ujauzito. Mlongo wa kwanza wa ujauzito ni miezi mitatu ya mwanzo tangu ushike mimba, pia inajulikana kama wiki ya 1 kuendelea mpaka wiki 12. Wakati wa kipindi hichi mwili wako unaanza mabadiliko mbalimbali, kati ya dalili halisi za mimba ni pamoja na kujisikia kutapika, uchovu wa ajabu, kuumwa kwa mgongo, kubadilika kwa tabia ghafla na stress. Hizi zote ni kawaida kwa mama mjamzito wakati wa wiki ya 1 hadi 12 ya mimba. Kwa bahati nzuri, nyingi ya dalili hizi huwa zinapotea unapoingia kwenye mlongo wa pili wa ujauzito. Unashauliwa kuacha kuvuta sigara na kunywa pombe wakati ukiwa mjamzito, kwani tabia hizi zinaweza mduru mtoto akiwa tumboni.

Wanawake wengi huenda kuona waganga wao (doctors) kipindi hiki cha mlongo wa kwanza mara nyingi wiki ya 8 hadi 10, hii ni vizuri kwani ndio wakati wa muhimu sana kwa mtoto kukuzwa vizuri tumboni. Mganga wako atakuelewesha na kuchukua vipimo vinavyotakiwa kuhakikisha kama kweli una mimba. Wanawake wengi wanaweza pia kusikia mapigo ya moyo ya mtoto akiwa karibu wiki 12 tumboni, ingawa inaweza chukua muda zaidi kwa wanawake wengine.

Wiki ya 1 na 2

Wiki hii ni mara ya mwisho kuona siku zako kabla hujagundua kwamba una mimba. Furahia! sawa, labda hautafurahia kutegemea na matakwa yako. Basi, hiki ni kipindi cha kuaga yale maumivu ya siku (period pains) mpaka utakapojifungua. Kwa wiki hizi mbili za mwanzo mimba bado hata haijashika kwanza. Wakati mganga wako anapohesabu siku yako ya kujifungua huwa anahesabu wiki 40 kuanzia siku yako ya kwanza ya kuona mwezi(period) kabla tuu ya kushika na mimba. Na sio kuanzia siku mimba iliposhika (mara nyingi ni siku ya 14 baada ya kuona mwezi).

Kipindi hiki yai linajiandaa kushuka ili kukutana na mbegu za kiume kutunga ujauzito. Kama unapanga kupata ujauzito, sasa ni wakati muafaka wa kuacha sigara na pombe, pia unaweza anza kunywa vidonge vya vitamin na folic acid, ambavyo husaidia mtoto asipate magonjwa ya ubongo akiwa tumboni.



Kipindi hichi mwili unatoa hormone zinazoitwa estrogen na progesterone kwa kuuandaa mwili kwa ajili ya siku(period), wakati ovaries zinaporuhusu yai kutoka. Kama ni bahati yako, yai hili ndilo litatunga ujauzito na kusafilishwa kwenda kwenye falopian tube mpaka kwenye uterus na hapo litakaa kwa wiki 40 likitunga mtoto.