Contact demartitis ni ugonjwa wa uvimbe wa ngozi ambao hutokea wakati unapogusa kitu .
Huu ni ugonjwa wa aina ya eczema ambayo unaweza kusababisha ngozi kuwasha na kuwa na magamba, wakati mwingine kuhisi kuungua na kuchoma. Husababisha ngozi kuwa na mapele yenye maji ambayo huchubuka, kuwa kavu na kupasuka.
Inaweza kuathiri sehemu yoyote ya mwili lakini kwa kawaida huathiri mikono.
Kusoma zaidi juu ya dalili za ugonjwa huu bonyeza http://www.nhs.uk/Conditions/Eczema-%28contact-dermatitis%29/Pages/Symptoms.aspx
Ugonjwa huu husababishwa na:
- kikereketa (Kitu kinachosababisha kidonda kwenye ngozi), au
- allergen (Kitu kinachosababisha mfumo wa kinga mwilini kupigana matokeo yake huathiri ngozi)
Kutibu Contact Dermatitis
Hata hivyo, hii haiwezekani wakati wote, hivyo matibabu ya kutumia emollients yanahitajika. Imollients ni mafuta yanayosaidia kutopotea kwa maji ngozini. Madawa ya steroidi yanaweza kutumika kutibu dalili kali.
Baada ya matibabu, watu wengi wenye ugonjwa huu hupata nafuu na hatimaye kupona. Hata hivyo, baadhi ya watu wanaweza kupata matatizo, dalili kali ambayo kuathiri ubora wa maisha yao.
No comments:
Post a Comment