Saturday, 8 November 2014

Ugonjwa wa kifafa (seizures) kwa watoto


Kifafa mara nyingi husababishwa na uvujaji wa wave za kama za umeme (electrical discharge) kwenye ubongo ama husababishwa na hali ya kuzimia (baada ya kupunguka kwa msukumo wa damu ubongoni). Dalili (symptoms) zinaweza hutofautiana kulingana na sehemu ipi ya ubongo imehusika, lakini mara nyingi utasikia hali ya mwili kusisimka sio kwa kawaida, misuli kuvutika/kukaza yenyewe, na pia kupoteza fahamu.
Baadhi ya vifafa vingine huwa ni matokeo ya magojwa mengine mwilini, kama upungufu wa sukari kwenye damu, maambukizi, kuuumia kichwa(head injuries), ajari za barabarani au kuoverdose madawa ya kulevya.  Pia kifafa kinaweza sababishwa na uvimbe kwenye ubongo ama tatizo linguine la afya linaloathiri ubongo. Kifafa mara nyingi hutokea zaidi ya mara moja.

Watoto wa chini ya miaka 5 huwa wanapata hali ya kifafa pale joto lao la mwili linapozidi degree 38 (100.4° F (38° C) aina hii ya kifafa inaitwa  Febrile seizure. Hii inaogopesha kama mzazi lakini hii hali ni ya dakika chache tuu, mara chache husababisha matatizo makubwa, especially kama joto hili limesababishwa na maambukizi kama meningitis.

Kwa watoto chini ya miaka 5, kuhold pumzi inaweza sababisha hali ya kifafa (seizure). Kuna watoto wakati wanapokasirika huwa wanashikiria pumzi (hawavuti pumzi kwa sekunde chache) kabla tuu ya kuachia kilio kikubwa, kabla ya kupoteza fahamu kifafa kufuatia. Mara nyingi hali hii huisha yenyewe.

Watoto wa umri zaidi ya miaka 5 wachache huwa na hali hii lakini mara nyingi huwa inaisha baada ya sekunde chache.

Kama mtoto wako ana kifafa ufanyeje
Kama mtoto wako amepatwa na kifafa basi unashauriwa kumlaza chini sehemu ambayo ni salama, wanashauri umlaze upande wake wa kulia. Ondoa kitu chochote cha hatari ambacho kipo karibu, kama vyupa, sindano, mawe n.k. Kama ana cheni shongoni ivue ama kama nguo ipo shingoni ivue pia isimkabe.  Usijaribu kupanua mdomo wa mtoto anapokuwa na kifafa ama kuweka kitu mdomoni kwake, pia usijaribu kuzuia kuweweseka kwake.
Mara tuu kifafa kinapoisha basi mfariji mtoto, ni muhimu kwa watoto kubaki kulala chini mpaka hali hii iishe kabisa nay eye mwenyewe akitaka kuinuka.
Tafadhari mwite daktari pale ambapo kifafa kinaendelea zaidi ya dakika 5, pia kama mtoto ana vitu vifuatavyo:
       . anashindwa kupumua
       .ameumia kichwa
       .ana magonjwa ya moyo
       .hajawahi kupata kifafa zamani
       .kama amekunywa sumu ama ameoverdose dawa.

Baada ya kifafa, mtoto huonekana kuchoka, amechanganyikiwa, na anaweza kulala usingizi mzito sana (postictal period) hauhitaji kumwamsha mtoto as long as anapumua vizuri. Usijaribu kump chakula mpaka mtoto aamke na aonekane kuchangamka.

Baada ya kifafa mtaarifu daktari kuangalia tatizo lililosababisha hiyo hali ni nini.








Sunday, 5 October 2014

Tatizo la Kutokulala kwa watoto wachanga

Watoto wengi wadogo huwa wanapata shida sana kutulia na kulala wakati wa usiku. Kwa watu wengine hili sio tatizo kwao na kama haikusumbui mtoto wako kwenda kulala muda ambao wewe unaenda kulala, basi sio shida. Lakini, kama wewe, ama mtoto wako anasumbuka na tatizo la kushindwa kulala usiku unaweza kujaribu kufanya yafuatayo:

Kila mtoto ni tofauti na fanya tuu kile unachoona kinafaa kwa mwanao.


Kama Mtoto wako hataki kwenda kitandani:

  • Amua saa ngapi ama mda gani unataka mtoto awe anaenda kitandani.
  • Kwa kuanza, mda wa mtoto kwenda kulala ukikaribia (ule mda anaolalaga kila siku) anza kumpeleka kulala dakika 20 kabla kwa siku ya kwanza, alafu siku ya pili mpeleke dakika 30 kabla, ya tatu iwe dakika 40 kabla na kuendelea kuongeza dakika 10 kila siku mpaka ifikie mda ule unaotaka wewe.
  • Jipangie kikomo cha kukaaa na mwanao kitandani wakati wa kulala, mfano msomee hadithi moja tuu, alafu sema usiku mwema, muage na kumwacha alale.
  • Mpatie mtoto wako toy yake anayoipenda alale nayo, mfano kama huwa anatumia dummy ya mdomoni, ama kitaulo (kuna watoto hunyonya kitaulo) ama chochote kitakachombembeleza kulala. 
  • Kama mtoto wako analia, umwache kitandani na uondoke chumbani na mpatie dakika 5 mpaka 10 ya kujituliza mwenyewe kabla ya kumyamazisha tena.
  • Usimnyanyue ama kumbeba mtoto, ama kumtoa kitandani na kama mtoto atainuka na kutoka kitandani basi mchukue na kumrudisha kitandani tena.
  • Washa taa yenye mwanga mdogo (kama unayo) ama acha mwanga wa mbalamwezi uingie kama kutakuwa na ulazima huo.
  • Hakikisha amelala kabla ya kwenda kumwangalia mtoto ili usimwamshe tena.
  • Fanya hivi kila siku na usikate tamaa baada ya siku moja tuu, jipatie siku 5 ili mtoto awe na mazoea.

Kama mtoto anaamka mara kwa mara usiku.

 Ni kawaida kwa watoto wa zaidi ya miezi 6 kulala usiku mzima bila kuamka, Hata hivy, kuna watoto wengi  chini ya miaka mitano huwa hawalali usiku mzima bila kuamka. Kuna ambao watarudi kulala tena wao wenyewe na wengine ambao watalia kwa kutaka uwepo wa mtu.

Kama hii hali itatokea, jaribu kutatua tatizo linalimfanya mwanao aamke usiku.
Je ni njaa? kama mwanao ni mkubwa zaidi ya mwaka moja, maziwa na uji huwa yanaweza mfanya alale usiku mzima kama hivyo ndio alikunywa mda tuu kabla ya kulala.

Je ni uoga/hofu ya giza? unaweza kutumia taa za usiku ama unaweza acha taa ya corrido iwake usiku.

Je ni ndoto mbaya? kama ni hivyo jaribu kutafuta kama kuna kitu kinachowasumbua ambacho ndio husababisha kuota usiku.

Je ni joto/ baridi kali? kama ni hivyo punguza ama uongeze nguo za kujifunika ama punguza/ongeza joto ama baridi kwenye chumba kwa kufungua milango ama kupunguza AC.



Kama hakuna sababu maalumu inayomfanya mwanao aamke, alie ama kutaka ukae nae usiku basi jaribu yafuatayo:

  • Mda wa kuamka - kama mwanao huamka wakati huo huo kila usiku basi jaribu kumwamsha kati ya dakika 15 mpaka 60 kabla alafu mbembeleze tena kurudi kulala. 
  • Mruhusu mtoto alale chumba kimoja na kaka yake ama dada yake kama tatizo ni kuogopa kuwa peke yake. Hii itawasaidia wote walale usiku mzima.
  • Mfundishe mwanao kujirudisha kulala yeye mwenyewe usiku, kwanza kama kila kitu kiko sawa, mmbembeleze mwanao kulala bila ya kuongea nae sana akiwa kitandani. Kama anataka kinywaji mpe maji ila angalisho usimpatie chakula wakati akiwa ameshtushwa na usingizi. Ili njia hii ifanye kazi ni lazima  umwache mtoto kitandani na usimnyanyue na kwenda nae sebuleni, ama chumbani kwako. Mwache alie kwa kati ya dakika 5 hadi 10 ndipo ukamwangalie tena. Mwambie arudi kulala na mwakikishie kwamba hakuna kitu cha kuogopesha na usiongee nae kitu kingine, kama ni mtoto mchanga mbembeleze kwa kumpapasa mgongoni akiendelea kulia mbebe kwa dakika 2 tuu alafu mrudishe kitandani.  mwache kama analia ikifika dakika 10 nenda tena, fanya kama hapo juu na umwache ena ajirudishe kulala. Endelea hivyo kwa siku kadhaa na mtoto atazoea na kuanza kusinzia mwenyewe ukimweka kitandani. 
  • Msaidiane na mumeo, mnaweza mkafanya zamu ya kumwangalia mtoto anapolia, hii pia husaidi mtoto kuwajua na kuwazoea wazazi wote wawili, pia itamfanya mama asichoke sana.

Ndoto za kutisha



Ndoto za kutisha ni kawaida kabisa. Wao mara nyingi huanza kati ya umri wa miezi 18 na miaka mitatu. Ndoto hizi ni si kawaida ni ishara ya masumbuko ya hisia. Huwa inaweza kutokea kama mtoto wako ana wasiwasi juu ya kitu au amepata hofu na kipindi ama hadithi aliyoangalia kwenye luninga.  Baada ya ndoto, mtoto wako atahitaji faraja na uhakika. Kama mtoto wako anaota ndoto hizi sana na hujui ni kwa nini basi ongea na daktari.
 
Kuweweseka usiku

Hutokea kabla ya umri wa mwaka moja ingawa pia ni kawaida zaidi kwa watoto kati ya umri wa miaka mitatu hadi nane. mara nyingi mtoto huweweseka na kupiga kelele ama kupigapiga mikono na miguu akiwa bado yupo usingizini. hutokea baada masaa machache ya kulala, wanaweza kukaa na kuongeaongea wakiwa usingizini na kuonekana wenye hofu wakiwa usingizini. Wala usiogope na mtoto wako itafika wakati itapita tuu.

Usimwamshe mwanao wakati akiweweseka ila kama hutokea mda huohuo kila usiku basi jaribu kumwamsha dakika 15 kabla ya muda ule anaoweweseka kila siku. abaki macho kwa dakika chache kabla ya kumrudisha kulala tena.



I hope hayo maelezo hapo juu yamesaidia, pia angalia mtoto kutokulala usiku







Tuesday, 30 September 2014

Ugonjwa wa vipele kutokana na nappy za kutupa (mapampas)

Leo nimeona tujulishane na kubadilishana mawazo kuhusu hili suala la allergy ya diapers (tunayaita mapapas) kwa watoto wetu. Kutokana na mabadiliko ya kimaendeleo siku hizi sio kama zamani watotot wetu yumezowea kuwavalisha chupi/ nappy za kutupa, yaani zikishajaa mikojo hatufui tena badala yake unazitupa.

Vipele kutokana na diapers ni kawaida kwa watoto na sio ishara ya kumtelekeza mtoto. Huu ni ugonjwa wa ngozi amba unatokana na kugusana na kitu ambacho husababisha allergy na matokeo yake vipele hutokea. Angalia picha zifuatazo:

Huu ugonjwa husababishwa na bacteria ama fangasi ambao kwa kawaida huwepo kwenye ngozi ya mtoto.

Kumbadilish mtoto diaper mara kwa mara inasaidia kupunguza vichochezi kwa allergy hii.  Vichochezi huwepo kwenye ngozi ya mtoto.

Mtoto anapokuwa na ugonjwa huu jitahidi kuacha kutumia baadhi ya mafuta ama creams ambazo zisizopitisha hewa kuingia kwenye ngozi (mfano, petrolium jelly, mafuta ya mgando ya kupaka) na wakati mwingine antifungal cream, low-potency hydrocortisone cream. High-potency steroid creams, powders, na baking-soda/boric-acid baths and neomycin-containing ointmentspia ni za kuziepuka.












 Nini husababisha vipele vya diaper

Kuna makundi kadhaa ya sababu wa ugonjwa huu wa ngozi Kwanza kabisa ni "kikereketa" au "kugusana(contact)"  Ngozi huonekana nyekundu (kama vile imechomwa na jua) alafu hubadilika na kuwa na tabaka (layer) juu wa ngozi. Tofauti ya ugojwa huu na magonjwa mengine ya ngozi ni kwamba utagundua kutokuwepo kwa vipele sehemu zenye mikunjo kwenye ngozi ya mtoto (matakoni), hii inaonyesha kwamba mkojo na kinyesi huchangia kwani mikojo na kinyesi huwa na wadudud wa bacteria na fungus. Mikojo na kinyesi huwa hazifiki sehemu zenye mikunjo na ndio maana hakuna wadudu hawa, hivyo vipele huwa havionekani sehemu hizi

Bacteria aina ya (Staph na Strep) na fungus aina ya candida mara nyingi ndio huonekana kwenye ugonjwa wa diaper. Kama imesababishwa na bacteria basi huanza kwa kusababisha vipele vidogodogo (Impetigo) ambavyo huja kuwa malengelenge na kupasuka na kujisambaza, matakoni na sehemu za karibu,  hii husababisha  kuwashwa kwa ngozi.

Kama imesababishwa na fungus basi huoneka ngozi madoa madoa  myekundu na ukubwa (kati ya 2mm - 4mm). Mara nyingi huonekana karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa. 

Ugonjwa huu ni rahisi kuujua kwa macho tuu, ukiwa na tatizo mpeleke mtoto kwa daktari. 

Vikereketa mara nyingi hutokana na harufu na material ya diaper. Ingawa ni mara chache sana allergy ndio sababu ya ugonjwa huu, lakini kama ukiona tatizo ni diaper basi badilisha diper. Pia ikiwezekana jaribu kutumia wipes zisizo na harufu.

Tufanyeje?


Dawa kubwa ni kuzuia mtoto asipate huu ugonjwa, nimelist vitu vya kufanya kama ifuatavyi:

1. Wewe kama mzazi (mama ama baba) unatakiwa kumkagua mtoto kila siku, nasema hivi sababu wazazi wengi huwaachia mabinti wa kazi kulea mtoto na  hujisahau majukumu yao kama wazazi. Hi itasaidia kuona kama ugonjwa huu unapoanza.

2. Jitahidi kumuogesha mtoto asubuhi na kabla hajaenda kulala, hii mara nyingi husaidia safisha kikereketa ambacho kilibaki kwenye diaper (ikiwezekana msafishe mtoto na maji kila unapombadilisha diaper badala ya kutumia wipes) Wipes zitumike pale ambapo maji hakuna.

3. Upele unapotokea, msafishe na maji na nguo safi na laini na sio wipes. 


Kwa maelezo zaidi tembelea zifuatazo

Hapa na hapa 




















Tuesday, 17 June 2014

Ugonjwa wa vipele vya nappy kwa watoto

Vipele vya nappy ni ugonjwa wa kawaida kwa watoto, huwa vnasababishwa baada ya ngozi ya mtoto napokutana na mkojo ama mavi ambayo yanabebwa na nappy.

Vipele hivi hufanya ngozi ya matakoni ya mtoto kuvimba, ngozi ya matakoni  huwa imezungukwa na vipele. Ikitokea hivi utahitaji kumbadilisha nappy mara kwa mara.

Vipele hivi zinaweza kutibiwa kwa cream unaweza ipata toka pharmacy. Unaweza kuacha kutumia wipes mpaka vipele vitakapopona kabisa.

Ugonjwa wa ngozi watoto


Contact demartitis ni  ugonjwa wa uvimbe wa ngozi ambao hutokea wakati  unapogusa kitu .

Huu ni ugonjwa wa aina ya eczema ambayo unaweza kusababisha ngozi kuwasha na kuwa na magamba, wakati mwingine kuhisi kuungua na kuchoma. Husababisha ngozi kuwa na mapele yenye maji ambayo huchubuka, kuwa kavu na kupasuka.







Inaweza kuathiri sehemu yoyote ya mwili lakini kwa kawaida huathiri mikono.

Kusoma zaidi juu ya dalili za ugonjwa huu bonyeza http://www.nhs.uk/Conditions/Eczema-%28contact-dermatitis%29/Pages/Symptoms.aspx

Ugonjwa huu husababishwa na:

  •      kikereketa (Kitu kinachosababisha kidonda kwenye ngozi), au
  •      allergen (Kitu kinachosababisha mfumo wa kinga mwilini kupigana matokeo yake     huathiri ngozi) 



Kutibu Contact Dermatitis

Kama unaweza kufanikiwa  kuepuka kikereketa (irrritants) au allergener zinazosababisha contact dermatitis basi hali yako itapona.

Hata hivyo, hii haiwezekani wakati wote, hivyo matibabu ya kutumia emollients yanahitajika.  Imollients ni mafuta yanayosaidia kutopotea kwa maji ngozini.  Madawa ya steroidi yanaweza kutumika kutibu dalili kali.

Baada ya matibabu, watu wengi wenye ugonjwa huu hupata nafuu na hatimaye kupona. Hata hivyo, baadhi ya watu wanaweza kupata matatizo, dalili kali ambayo kuathiri ubora wa maisha yao.

 


Tuesday, 11 June 2013

Mtoto miezi 6 mpaka 12


Rudi mtoto chini ya miezi 6

Mtoto miezi 6 mpaka 12

Mpaka wa 6, mtoto anaweza kulala muda wa masaa 3 wakati wa mchana na kulala zaidi ya masaa 9 hadi 11 wakati wa usiku. Katika umri huu, unaweza kumuacha alie usiku, hii ni kwa watoto wachanga ambao huamka na kulia wakati wa usiku.

Wazazi wanaweza kuwapatia watoto muda kidogo watulie na kujirudisha kulala wao wenyewe bila kubembelezwa. Kama huwezi kumwacha mwanao akilia basi mbembeleze bila kumbeba kwa kumuongelesha akiwa kitandani huku unamsugua (rub) mgongoni kidogokidogo, alafu muache uondoke akijua kwamba anatakiwa kurudi kulala - isipokuwa kama anonekana kuwa mgonjwa. Watoto wagonjwa wana haja ya kubebwa na kutunzwa. Kama mtoto wako haionekani mgonjwa na anaendelea kulia, unaweza kusubiri kwa muda mrefu kidogo, kisha rudia tena kumwacha ajibembeleze yeye mwenyewe atakapolia tena.

Kati ya miezi 6 na 12, wasiwasi wa kutengana toka kwa mama humpata mtoto, hii ni kawaida na ni sehemu ya ukuaji ya mtoto. Sheria ni ileile, jaribu kutombeba mtoto wako, kutomwashia taa, kutomwimbia, kutomwongelesha, kutocheza nae, au kulisha mtoto wako wakati anatakiwa alale. Hizi zote hazitamruhusu mtoto wako kujifunza kulala mwenyewe na ataendelea kuamka usiku.

Watoto chini ya miaka 3
Kuanzia mwaka 1 hadi 3, wengi wachanga kulala masaa 10 hadi 13. Kujitenga wasiwasi, au tu hamu ya kuwa pembeni na mama na baba (ili asimiss kitu), inaweza kuwahamasisha mtoto kukaa macho.

Wazazi wakati mwingine kufanya makosa ya kufikiri kwamba kumwacha mtoto asilale mapema kutamfanya mtoto alale zaidi usiku. Kiukweli, ingawa, watoto wanaweza kuwa na wakati mgumu kulala kama wamechoka sana. Ingawa watoto hulala kidogo mchana, usimlazimishe alale mchana kama hataki, lakini ni muhimu kuwa na ratiba ya muda wa utulivu kwa mtoto, akae chumbani kwa mda hata kama kataki kulala mchana.

Kuanzisha utaratibu wa kwenda kulala husaidia watoto kupumzika na kuwa tayari kwa ajili ya usingizi. Kwa mtoto, utaratibu unaweza kuwa toka dakika 15 hadi 30 na ni pamoja na shughuli za kutulia kama vile kusoma hadithi, kuoga, na kusikiliza muziki laini.

Chochote utakachofanya, mwanao anatakiwa ajue ni usiku na anatakiwa alale, usibadilishe mpangilio ulouweka kila siku kabla ya kulala.  Kila inapowezekana, mruhusu mwanao achague nini anataka usiku huo, yaani kama ni hadithi, ama kuimbiwa, nguo  gani ya kulalia anataka, toy ipi ya kulala nayo anataka, nyimbo iipi, hadithi ipi n,k ilimradi bado mtafuata mpangilio uleule kila siku. Hii inamfanya anaona ana udhibiti kwenye huu mpangilio.

Lakini hata mtoto mlalaji  huwa anaamka mara moja moja. Kuota meno kunaweza  kumuamsha pia ndoto. Ndoto huanza katika umri huu, na kwa watoto wadogo, ndoto inaweza kuwa ni kutisha. Jinamizi ni hasa inatisha kwa watoto, ambao hawawezi kutofautisha mawazo na ukweli. (Basi kuwa makini kuchagua programu gani mwanao anaangalia  kabla ya kwenda kulala)


Kuwafariji na kushikilia mtoto wako kwa nyakati hizi. Kuwa na majadiliano juu ya ndoto kama yeye anataka, na kukaa hadi mtoto wako ni atulie. Kisha muhimize mtoto wako arudi kulala mapema iwezekanavyo.

Mtoto kutolala usiku

Je mwanao huwa ana tabia ya kuamka usiku? 
Huwa anakufuata chumbani kwako?
Anataka kulala pembeni yako?

Watoto wanapokuwa wachanga huwa wananyonya maziwa ya mama ama ya chupa kila baada ya masaa machache. Hivyo mazoea ya kuamka usiku kwa ajili ya kunyonya huwa yanaendelea pindi mtoto huyo anapokuwa na umri wa kuweza kulala usiku bila kutegemea chakula. Hii huwa inatokana na mzazi/wazazi kuiendeleza iyo tabia kwa kumpatia mtoto maziwa usiku. mtoto pindi anapoanza kuanza kula chakula kigumu         basi unaweza kuanza kumtoa kwenye kunyonya usiku polepole mpaka ataweza kulala mwenyewe usiku mzima bila kuamka.

Kama unataka kurekebisha hiyo tabia unaweza kufanya yafuatayo:

Kiasi gani cha usingizi kinatosha kwa mwanao?

hii inategemea na umri wa mtoto na mtoto mwenyewe. Watoto wapo tofauti, Hermes anaweza kulala toka saa 2.00 usku mpaka saa 2 asubuhi, wakati Henrick yeye ni mtoto wa maluelue analala atalala kuanzia saa 3 usiku na kuamka saa 12 asubuhi. utamjua mwanao kama ana usingizi/anakosa usingizi mara tabia zake zikichange, anaweza kuwa juu juu, mbishi na analialia.  hizi chini ni masaa ya kulala kwa mtoto kutegemeana na umri wake:

Watoto chini ya miezi 6

Hakuna formula ya kulala kwa ajili ya watoto wachanga  kwa sababu saa zao mwilini hazijakamilka bado. Wao kwa ujumla huwa wanalala au drowse kwa masaa 16 hadi 20 kwa siku, hii ni kati ya usiku na mchana.

Watoto wachanga lazima waamshwe kila baada ya masaa 3 na 4 hadi uzito wao uwe imara, ambapo kwa kawaida hutokea ndani ya kipindi cha wiki moja. Baada ya hapo ni sawa kama mtoto akilala kwa muda mrefu zaidi.
Baada ya wiki chache za mwanzo, watoto wachanga wanaweza kulala kwa muda mrefu kama masaa 4 au 5  huu ndio muda ambao matumbo yao madogo yanaweza kumudu kati ya ulishaji. Kama watoto hulala vizuri wakati wa usiku, basi watakula zaidi wakati wa mchana.

Wakati tu wazazi wanapohisi kuwa kulala usiku kunaonekana kama ndoto ya mbali, usingizi wa mtoto wao kawaida huanza kuhama kuelekea usiku. Anapokuwa na miezi 3, mtoto hulala kwa wastani wa masaa 13 katika kipindi cha saa 24 (yale masaa 4-5 ya kulala wakati wa mchana  huvunjwa katika kulala mara mojamoja(naps) na masaa 8-9 wakati wa usiku. Asilmia 90% ya watoto wa umri huu hulala usiku mzima, kwa maana ya masaa 5 hadi 6 katika mfululizo.

Lakini ni muhimu kutambua kuwa watoto hawawi macho saa zote, wakati wanasikika kama wapo macho, wao wanaweza kulia na kufanya kila aina ya kelele nyingine wakati wa usingizi wa mang'amung'amu. Hata kama wakiamka usiku, wanaweza tu kuwa macho kwa dakika chache kabla ya kurudi tena kulala wao wenyewe bila kubembelezwa. 

Kama mtoto chini ya umri wa miezi 6 anaendelea kulia, ni vizuri kwenda kumsikiliza. Mtoto wako inawezekana kuna kitu kinachomfanya alie, njaa, joto, amekojoa, baridi, au hata mgonjwa. Lakini mara kwa mara usiku kumuhudumia mtoto usiku kwa ajili ya kumbadilisha na kumlisha lazima iwe ya haraka na kimyakimya. Kipindi hiki usifanye chochote kile kitakachomwamsha mtoto kama kuzungumza, kucheza, au kuwasha taa. Muhimiza kwamba ni usiku na ni kwa ajili ya kulala. Unamfundisha hili kwa sababu mtoto wako hajali ni muda gani ilimradi mahitaji yake yanakamilishwa.

Kimsingi, mtoto wako lazima awekwa kwenye kitanda kabla ya kuanza kusinzia. Na si mapema mno kuanzisha kamchezo cha kwenda kulala mda fulani kila siku, unaweza kumzoesha kumwimbia kabla ya kilala, fanya mfululizo na katika utaratibu huo kila usiku.

Lengo ni kuwafanya watoto walale kwa kujitegemea, na kujifunza kujibembeleza wenyewe na kurudi kulala pindi wanapoamka usiku wa manane.

Angalia mtoto miezi 6 mpaka 12